Latest Posts

DC MAGOTI: SIJAZUIA NGOMA KISARAWE

Baada ya kunukuliwa kwa nyakati tofauti akipiga marufuku ngoma ya unyago, Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Petro Magoti, amesema hajazuia ngoma za asili ambao ni utamaduni wa jamii ya wazaramo wanaopatikana katika wilaya hiyo.

Magoti amesema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari akitangaza ujio wa tamasha la ‘Bata Msituni’ linalolenga kutangaza vivutio vya utalii litakalofanyika katika msitu wa hifadhia asilia ya Pugu kazimzumbwi.

“Tamasha hili linalengwa kuwakutanisha watu pamoja, wa-sociolize, tunahitaji kubadilishana mawazo, kubadilishana uzoefu, kujifunza. lakini pili kuonesha utamaduni wa wazaramo katika wilaya ya kisarawe, kama mnavyojua kwamba wazaramo wanangoma, watu walisema Magoti (Yeye Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe) amezuia ngoma! Mimi sijazuia ngoma na hapa sasa tunaleta ngoma, tutakuwa na ngoma tano za Wazaramo hapa zitarindima ili wazungu waje waone kwamba jinsi gani Wazaramo watu wa Pwani wanajua kucheza ngoma”.

Miongoni mwa ngoma za asili alizotaja zitakuwepo ni, Vanga, Tokomire, Dogori, Mdundiko pamoja na Msewe.

Tamasha hilo litatarijia kufanyika mwezi Septemba kuanzia tarehe 03 hadi 09, huku likijumuisha washiriki kutoka mataifa matatu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!