Latest Posts

Kufuatia shambulizi la ulipizaji kisasi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Israel, viongozi wa nchi kadhaa za Afrika wametoa wito wa kujizuia kwa Israel baada ya shambulio la Iran.

Kufuatia shambulizi la ulipizaji kisasi la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa Israel, viongozi wa nchi kadhaa za Afrika wametoa wito wa kujizuia kwa Israel baada ya shambulio la Iran. Afrika Kusini, Nigeria, Kenya, Somalia na nchi nyingine kadhaa za Afrika zimeitaka Israel kujizuia wakati baraza lake la mawaziri la vita likikutana ili kuamua iwapo italipiza kisasi dhidi ya shambulio la anga la Iran ambalo halijawahi kushuhudiwa. Rais wa Kenya William Ruto ameitaka Israel kujizuia kwa kuzingatia hitaji la dharura la pande zote kujiondoa katika mapigano ambayo yanaweza kuwa vigumu sana kumalizika. “Shambulio la Iran linawakilisha tishio halisi la amani na usalama wa kimataifa” alisema Ruto Wizara ya Uhusiano wa Kimataifa na Ushirikiano ya Afrika Kusini imesema katika taarifa yake kuwa si jambo la busara kukimbilia vita kwani ni watu wa kawaida wanaoteseka kutokana na mizozo. Nayo Wizara ya Mambo ya Nje ya Nigeria imezitaka Israel na Iran kutafakari juu ya kujitolea kwa wote katika utatuzi wa migogoro kwa njia ya amani. Iran na Israel kwa pamoja hazijawa na uhusiano wa muda mrefu wa kisiasa na mataifa ya Kusini mwa jangwa la Sahara, huku uhusiano wa nchi hizo mbili na nchi za kanda hiyo ukiwa umedhoofika kutokana na mahusiano yake mabaya na nchi za kiarabu kwa ujumla na hasa kuhusu suala la Palestina.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!