Latest Posts

DED MILLAO AWATAKA WANAFUNZI SHULE MPYA YA MNENIA SEKONDARI KUFANYA VIZURI

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma, Shaban Millao amewataka wanafunzi wa shule mpya ya Mnenia Sekondari kufanya vizuri kwenye mitihani yao na kuhakikisha kwamba wanapata Daraja la Kwanza (Division One) wote kwani wao ndio wanafunzi wa kwanza hivyo wanapaswa kuacha baraka itakayofuatwa na vizazi vijavyo.
 
DED Millao amesema hayo Februari 3, 2025 baada ya kufanya ziara ya kushtukiza katika Shule ya Sekondari Mnenia iliyopo Kondoa DC ili kujionea namna mambo yanavyokwenda.
 
Aidha Millao amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuipatia Mnenia kiasi cha Shilingi milioni 544.26 kwa ajili ya ujenzi wa shule hiyo na kufanya maisha ya wanafunzi hao kuwa rahisi kwani hapo awali walikuwa wakipaswa kutembea kilometa 7 kufuata elimu ya sekondari.
 
Aidha Mkurugenzi Millao amewataka walimu kufanya kazi yao ipasavyo kwa kujua kila mwanafunzi anavyoishi nyumbani akieleza kuwa baadhi ya wanafunzi wamebeba majukumu ya baba, mama warudipo nyumbani, hivyo waangalie namna ya kuwasaidia.
 
Kwa upande wao wanafunzi wamemuahidi Mkurugenzi kuwa watapambana kuhakikisha wanasoma na kufikia malengo yao kwani kikwazo cha umbali wa shule tayari kimeshatatuliwa na serikali inayoongozwa na Rais Samia.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!