Latest Posts

DHAMIRA YA KUMTUA MAMA NDOO KICHWANI YAZIDI KUSISITIZWA ARUSHA

Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, ameendesha kikao kazi na watumishi na watendaji wa sekta ya maji mkoani Arusha, akisisitiza umuhimu wa juhudi za pamoja katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za maji safi na salama.
 
Akizungumza katika kikao hicho siku ya Jumanne Desemba 03, 2024, Waziri Aweso amesema lengo kuu ni kuwahamasisha watendaji kuendelea kufanya kazi kwa bidii, kutoa huduma bora kwa wananchi, na kujitathmini kuhusu utekelezaji wa mipango na malengo ya sekta hiyo, ikiwa ni sehemu ya dhamira ya kumtua mama ndoo kichwani.
 
Waziri Aweso amewahimiza kuhakikisha kila mmoja anatimiza wajibu wake kwa weledi na kwa kuzingatia mahitaji ya wananchi, huku wakizingatia maelekezo ya kiutendaji ili kufanikisha malengo ya kitaifa katika sekta ya maji.
 
Miongoni mwa watendaji walioshiriki kikao hicho ni pamoja na wale wanaotoka Mamlaka ya Maji Arusha, RUWASA wilaya zote za Mkoa wa Arusha, Bonde la Pangani kanda ya Arusha, Bonde la Kati kanda ya Arusha na Kitengo cha Ubora wa Maji Mkoa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!