Latest Posts

GFA VEHICLE ASSEMBLER YASHINDA TUZO ZA RAIS KWA UUNGANISHAJI WA MAGARI NCHINI YA MWAKA 2024

Kiwanda cha kwanza cha kutengeneza na kuunganisha magari nchini Tanzania GF cha Vehicles Assemblers (GFA) kilichopo Kibaha mkoani Pwani kimeibuka mshindi kwanza kwa kampuni za kati nchini wakati wa utoaji wa Tuzo za Rais kwa Wazalishaji Bora (President’s Manufacturer of the year Awards – PMAYA) zilizofanyika jijini Dar es Salaam
 
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa tuzo hilyo Meneja mkuu wa Kiwanda hicho, Ezra Mereng amewapongeza wafanyakazi wake kwa umoja wao akieleza kuwa umoja hup ndiyo chachu ya mafanikio ya wao kukidhi ubora katika uzalishaji wa magari, na kwamba bila wao wasingweweza kufanikiwa katika ushindi.
 
Naye mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa kampuni hiyo, Salman Karmali amesema wao kama kampuni wanashukuru tuzo hiyo ambayo ni ya pili kwa kampuni ya GFA, na kwamba ni dalili mzuri kwani kiwanda hicho cha kuunganisha magari ndiyo kiwanda cha kwanza nchini Tanzania kuunganisha magari makubwa.
 
Mbali na kujivunia kuwa waongoza njia katika sekta ya usafirishaji nchini, Karmali alisema kutokana na mafanikio waliyoyapata kama GFA, wanaingia katika hatua ya pili ya upanuzi na uzalishaji ambapo wanatarajia katika upanuzi huo, watatengeneza magari kumi (trucks) kwa siku kutoka magari manne, na upanuzi huo utahusisha kuunganisha magari makubwa na madogo.
 
Ameongeza kuwa GFA inalenga kulifikia soko la Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika, jambo litakaloingiza fedha za kigeni kwa Taifa. Baadhi ya magari yanayozalishwa na GFA ni chapa za FAW, Hong Yan, na Foland.
 
Karmali pia amepongeza juhudi za serikali za kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji kupitia Sheria ya Local Content, ambayo imewezesha Watanzania kushiriki katika kazi mbalimbali migodini na miradi ya serikali, ambapo amesema sheria hiyo imeongeza vipato vya Watanzania wengi na kuwapa uwezo wa kununua magari kutoka kiwandani kwao Karmali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!