Latest Posts

HALMASHAURI YA SERENGETI KUKABILIANA NA UBOVU WA BARABARA

Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, mkoani Mara, imeweka mkakati wa kutenga fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya ujenzi, ikiwemo greda, ili kukabiliana na changamoto ya ubovu wa barabara katika wilaya hiyo badala ya kuendelea kutegemea wadau kila mwaka.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Serengeti, Dk. Maulid Suleiman, katika kikao cha Baraza la Madiwani cha Robo ya Kwanza ya mwaka, ambapo ametoa wito kwa baraza hilo kuidhinisha fedha hizo zitakapotengwa kwa ajili ya ununuzi wa greda.

“Tunaweza kutatua changamoto hii endapo tutakuwa na vifaa vyetu wenyewe badala ya kutegemea vifaa vya wadau, na miundombinu yetu itakuwa salama,” amesema Dk. Suleiman.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayubu Makuruma, ameongeza kuwa mshikamano miongoni mwa viongozi na wananchi utachangia kwa kiasi kikubwa katika kukabiliana na tatizo la ubovu wa miundombinu wilayani humo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!