Latest Posts

“HATUTAPIGIA MAGOTI UDHALIMU,” CHADEMA YAAPA KUTOPAMBA UKWELI KATIKA SIASA.

Katika kilele cha maadhimisho ya miaka 33 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Makamu Mwenyekiti wa chama hicho bara John Heche, amesisitiza kuwa CHADEMA haipaswi kutazamwa tena kama “chama kikuu cha upinzani,” bali kama chama kikuu nchini ambacho kimejipanga kuchukua hatamu za uongozi wa Taifa.

Akizungumza mkoani Mara, Heche amesema nguvu pekee itakayoweza kukidhibiti chama hicho ni mabavu ya vyombo vya ulinzi, kwani katika hoja na ushindani wa kisiasa, hakuna chama kinachoweza kusimama mbele ya CHADEMA.

Kiongozi huyo amewahakikishia wanachama kuwa uongozi wa sasa hautafanya usaliti wala kulegeza misimamo yake mbele ya udhalimu. Amesisitiza kuwa chama kitaendelea kusema ukweli bila kuupamba, bila kujali ukali wa mazingira ya kisiasa nchini.

“Hatutafanya usaliti, hatutamwonea mtu aibu. Kama ni nyeupe tutakuambia ni nyeupe, kama ni nyeusi hatutaipamba pamba. Hatutapigia magoti udhalimu.

Aidha Heche, amebainisha kuwa urithi mkubwa ulioachwa na muasisi wa chama hicho, Mzee Edwin Mtei, si jina la chama pekee bali ni mfululizo wa mapinduzi ya kisera ambayo yamebadilisha maisha ya Watanzania, ikiwemo kufutwa kwa kodi ya kichwa.

Amesema Mzee Mtei aliyefariki dunia Januari 19, 2026, nyumbani kwake Tengeru mkoani Arusha, alichagua jina la “Chama cha Demokrasia na Maendeleo” kwa makusudi ili kuakisi mrengo wa Kati-Kulia (Center-Right), unaoamini katika soko huru, haki za binadamu, na mamlaka ya wananchi.

“Kwa hiyo chama chetu ni chama cha mrengo wa kati kulia ambacho kinaamini katika demokrasia, kinaamini katika soko huru la watu kufanya biashara, unafanya bila bugha na serikali inatimiza wajibu wake unalipa kodi, tunaamini katika misingi ambayo rasilimali za nchi yetu zitumike kwa ajili ya kuendeleza watu wetu sio kuendeleza wageni. Hicho ndicho alichokipigania mzee Mtei”, ameeleza.

Heche ameeleza kuwa CHADEMA kimekuwa chachu ya mabadiliko makubwa ya kimaendeleo kupitia halmashauri kilizoziongoza:

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!