Latest Posts

HECHE AMJIBU KIHONGOSI SUALA LA YEYE KULIMA PARACHICHI

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche, amejibu mashambulizi ya maneno yaliyotolewa na Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, Kenani Laban Kihongosi, kuhusu shughuli zake za kilimo cha parachichi, akieleza kuwa anaweza kulima kwa mafanikio kwasababu ana mtaji wa kibinafsi uliomwezesha kuwekeza kwenye kilimo hicho.

Akizungumza leo, Septemba 24, 2026, katika mkutano wa hadhara uliofanyika wilayani Bariadi mkoani Simiyu, Heche amekiri kuwa ni kweli yeye ni mkulima mkubwa wa parachichi na mfugaji mzuri. Hata hivyo, ameeleza kuwa maendeleo yake kwenye kilimo na ufugaji yanasukumwa na fursa ya mtaji aliyoipata wakati alipokuwa mbunge, fursa ambayo kijana wa kawaida wa Kitanzania hana hadi Serikali itakapowajibika.

“Anasema ooh! anawaambia vijana wa Kitanzania sijui nini! Nini! yeye analima parachichi. Ni kweli, mimi ni mkulima mkubwa wa parachichi na ni mfugaji mzuri lakini mimi nafuga vizuri na nalima vizuri kwa sababu nina mtaji”, ameeleza.

Heche amebainisha kuwa badala ya viongozi wa CCM kukejeli maendeleo ya kibinafsi, wanapaswa kutambua kuwa ni wajibu wa Serikali kuweka miundombinu kama maji, matrekta, na mbegu bora ili kuwawezesha vijana na wananchi wengi kushiriki kwenye kilimo cha tija.

“Nimekuwa mbunge, nimechimba kisima shambani kwangu, kisima kirefu nimepandisha maji kwenye matenki. Parachichi zangu wakati wa jua zinamwagiliwa hazifi. Sasa wewe utalimaje? Kisima chenyewe kuchimba milioni 25 unaweza? Hiyo ni kazi ya serikali”, ameeleza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!