Latest Posts

IDADI YA ABIRIA UWANJA WA NDEGE WA SONGEA YAONGEZEKA

 

Baada ya maboresho makubwa yaliyofanywa katika uwanja wa ndege wa Songea kukamilika kwa asilimia 100 na kuanza kutumika, idadi ya abiria na safari za ndege zimeongezeka hatua ambayo inatajwa kuchochea ukuaji wa uchumi.

Idadi ya abiria imeongezeka kutoka abiria 3971 mwaka 2020 hadi kufikia abiria 19,260 mwezi Julai, makaa huu.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu Septemba 23, 2024 na Naibu Waziri wa Uchukuzi Mheshimiwa David Kihenzile kwenye mahojiano na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) mjini Songea mkoani Ruvuma akiwa kwenye ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Kihenzile ameongeza kwa kusema kuwa, ndege kubwa zinafanya safari mara tatu kwa wiki katika uwanja huo kwa siku za Jumatatu, Jumatano na Alhamisi.

Ameendelea kwa kusema kuwa, maboresho yaliyofanywa ni pamoja na kutengeneza njia ya kurukia na kutua ndege, maegesho ya ndege, mnara wa kuongozea ndege (control tower), njia za maungio.

Kwa upande wa jengo la abiria, Naibu Waziri huyo amesema

“Tunaliboresha jengo la abiria la sasa na wakati huo huo tuna mpango wa kujenga jengo lingine kubwa la abiria ili kuendana na maboresho ambayo yamefanyika katika uwanja huu”

Sambamba na hayo, ametanabaisha kuwa, uwanja mpya wa ndege unajengwa katika Mkoa wa Lindi kaa gharama ya zaidi ya shilingi bilioni 126 wakati huo wakiwa katika mchakato wa kutafuta eneo mkoani Njombe kwa ajili ya kujenga uwanja mpya wa ndege.

Kando na hayo, amesema hapo kesho Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka jiwe la msingi ujenzi wa bandari ya Mbamba bay, ujenzi ambao utagharimu zaidi ya shilingi bilioni 70 ambapo pia mkakati uliopo ni kuunganisha bandari hiyo na reli ya kisasa (SGR) kutoka bandarini hadi Mkoa wa Mtwara.

Akihitimisha amesema, mkataba wa maboresho makubwa ya reli inayotoka Dar es Salaam hadi Kapiri Mposhi nchini Zambia (TAZARA) umesainiwa wakati wa ziara ya Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan nchini chini hivi karibuni.

Maboresho makubwa kwenye reli hiyo yanahusisha kufumuliwa upya kwa reli hiyo ili kuongeza uwezo wa reli wa kubeba mizigo pamoja na kuongeza vichwa na mabehewa ya kutosha ya mizigo na abiria.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!