Latest Posts

IRAN YATOA ONYO KALI KWA MAREKANI: “TUTASHAMBULIA VITUO VYOTE VYA KIJESHI NA MELI ZENU KUKIWA NA UVAMIZI WA ARDHINI”

Taifa la Iran limeweka wazi mpango wake wa kulenga na kudhulu vituo vyote vya kijeshi pamoja na meli za Marekani endapo kutakuwepo na viashiria vyovyote vya uvamizi wa ardhini dhidi yao kutoka kwa nchi hiyo kubwa ya kimataifa.

Onyo hilo limetolewa na Kamanda mwandamizi wa Kikosi cha Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu (IRGC) nchini Iran, Ali Fadavi, siku ya Jumapili wakati akizungumza kupitia televisheni ya serikali, huku mvutano wa kijeshi kati ya mataifa hayo mawili ukizidi kushika kasi katika ukanda wa Mashariki ya Kati.

Fadavi, ambaye ni mkuu wa kundi la ushauri kwa kamanda mkuu wa IRGC, alisisitiza kuwa iwapo Marekani itaanzisha mashambulizi ya ardhini, Iran italizingatia na kulenga eneo au mali yoyote inayohusishwa na Marekani, zikiwemo kambi za kijeshi na vyombo vya majini, akidai kuwa Washington inafahamu vyema uwezo mkubwa wa makombora ya Iran katika kushambulia meli za kivita. Aliongeza kuwa uzalishaji wa silaha nchini humo kwa sasa unazidi kiwango kinachotumika, jambo linaloimarisha utayari wao wa kivita ikilinganishwa na vipindi vya nyuma.

Aidha, kamanda huyo alizungumzia hali ya usalama katika Mlango-Bahari wa Hormuz, akisema kuwa Iran na Oman zinapaswa kuandaa na kutekeleza sheria madhubuti zinazosimamia matumizi ya njia hiyo muhimu ya kimkakati. Alionya kuwa meli za Marekani zitakuwa hatarini kushambuliwa iwapo zitaendelea kupelekwa katika eneo hilo, akisisitiza kuwa uwepo mkubwa wa kijeshi wa Marekani unachochea zaidi mivutano.

Hata hivyo, hadi sasa Marekani haijasikika ikitoa tamko rasmi la moja kwa moja kujibu vitisho hivyo, lakini juhudi za kuongeza uwepo wake wa kijeshi Mashariki ya Kati zinaendelea kama hatua ya tahadhari, huku Rais Donald Trump akieleza kuwa uwezekano wa kuendelea na mashambulizi dhidi ya Tehran bado upo. Pande zote mbili zinaendelea kurushiana maneno ya onyo na vitisho vya kulipiza kisasi, huku utekelezaji wa kauli hizo ukitajwa kutegemea hatua zitakazochukuliwa na nchi hizo katika siku zijazo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!