Latest Posts

IRINGA WAJA NA “KITONGA MARATHON”, MSHINDI KUONDOKA NA SH. MILIONI 1.

Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa imekuja na mbio za “Kitonga Marathon”, zinazotarajiwa kufanyika Oktoba 31, 2026, pembezoni mwa Mlima Kitonga, kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji, utalii na kuhamasisha uhifadhi wa mazingira na maliasili za eneo hilo huku mshindi wa kwanza wa mbio za kilomita 21 akitarajiwa kuondoka na Shilini  milioni 1.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Fredy Makibete, amesema marathon hiyo ni fursa ya kuitangaza Kilolo na kuonesha fursa zilizopo katika sekta za kilimo, misitu, madini na utalii, kufafanua Serikali wilayani humo inavyolenga kuwafikisha wananchi na watu kutoka maeneo mbalimbali nchini kwenye fursa zinazopatikana Kilolo.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Siwema Jumaa, amesema mbio hizo zitahusisha kilomita 5, 10 na 21 pamoja na trail run ya Mlima Kitonga, inayolenga kukuza utalii wa asili na hiking.

Kwa upande wa zawadi, mshindi wa kwanza wa kilomita 21 atapata Sh1 milioni, wa pili Sh600,000 na wa tatu Sh400,000, huku kilomita 10 mshindi wa kwanza akipata Sh500,000, wa pili Sh300,000 na wa tatu Sh200,000 kwa wanawake na wanaume. Ada ya ushiriki ni Sh50,000 kwa kilomita 5, 10 na 21, na Sh70,000 kwa trail run.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!