Latest Posts

JESHI LA ISRAEL: TUMEZUIA MAKOMBORA SITA KUTOKA YEMEN NDANI YA WIKI MOJA

Jeshi la Israel limetangaza kuwa jeshi lake la anga limefanikiwa kuzuia makombora mawili yaliyorushwa kutoka Yemen siku ya Alhamisi kabla ya kuingia kwenye anga ya Israel. Ving’ora vya mashambulizi ya anga vilisikika katika miji ya Jerusalem, Tel Aviv, na maeneo mengine ya Israel ya kati kufuatia shambulio hilo, huku milipuko mikubwa ikisikika mjini Jerusalem baada ya ving’ora kulia.

Picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zinaonesha vipande vya roketi vikianguka katika mji wa Adh Dhahiriya, karibu na Hebron, kusini mwa Ukingo wa Magharibi unaokaliwa.

Shirika la utangazaji la Israel limeripoti kuwa mfumo wa ulinzi wa makombora wa Marekani wa THAAD ulishiriki katika kuzuia makombora yaliyorushwa kutoka Yemen kuelekea Israel. Aidha, televisheni ya Israel Channel 12 imeripoti kuwa maagizo yalitolewa kwa ndege iliyopangwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Ben Gurion ili kugeuza safari yake kuelekea Larnaca, Cyprus, sanjari na kuzuiwa kwa kombora.

Kwa upande wao, waasi wa Kihouthi wamesema kuwa walilenga uwanja wa ndege wa Ben Gurion na kambi ya kijeshi katikati mwa Israel kwa makombora mawili. Televisheni ya Al Masirah yenye uhusiano na Wahouthi imeripoti kwamba makombora mawili yaliyotumika ni kombora la balistiki la “Dhu al-Fiqar” na kombora la “Palestine 2” la hypersonic. Kituo hicho kiliongeza kuwa Wahouthi pia walilenga meli za kivita za “maadui” katika Bahari Nyekundu, ikiwa ni pamoja na meli ya kubeba ndege za Marekani Truman.

Mashambulizi haya yamekuja wakati ambapo Israel imeendelea na operesheni zake za kijeshi katika Ukanda wa Gaza takriban siku 10 zilizopita, huku kurushwa kwa makombora kutoka Yemen kikiwa kumeongezeka. Jeshi la Israel limeripoti kuwa ndani ya wiki moja iliyopita, limefanikiwa kuzuia makombora sita yaliyorushwa kuelekea nchini humo. Wahouthi wanadai kuwa mashambulizi yao ni hatua ya kuiunga mkono Gaza katika mgogoro unaoendelea Mashariki ya Kati.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!