Latest Posts

MABINTI WA VYUO VIKUU WAJIUNGA CCM, WAKIDAI CHADEMA KUNA MFUMO DUME

Kundi la mabinti kutoka vyuo vikuu mbalimbali nchini limetangaza kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) baada ya kudai kutoridhishwa na nafasi ya wanawake ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika jijini Dar es Salaam, mabinti hao waliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kampeni ya Mama Asemewe Taifa, Verynancy Mrema ambaye ameeleza kuwa uamuzi wa mabinti hao unatokana na CCM kuonesha kuthamini wanawake kwa kuwapatia nafasi za uongozi na maamuzi katika siasa na maendeleo ya taifa.

Akitolea mfano wa hali ilivyo ndani ya CHADEMA, mabinti hao wamekosoa vikali mfumo wa uongozi wa chama hicho kwa kudai kuwa unakandamiza wanawake na kuwatenga katika nafasi za maamuzi.

Mrema amesisitiza kuwa Kampeni ya Mama Asemewe itaendelea kuwa jukwaa muhimu la kuelimisha jamii kuhusu mchango wa wanawake katika maendeleo ya taifa, huku akimpongeza Rais Samia kwa kuendelea kuwa kiongozi wa mfano katika kuhakikisha wanawake wanapata nafasi sawa katika kila sekta.

Mkutano huo ulihitimishwa kwa mabinti hao kuahidi kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za kisiasa na maendeleo kupitia CCM, wakieleza kuwa chama hicho ni jukwaa sahihi la kuhakikisha sauti za wanawake zinapazwa na kusikilizwa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!