Latest Posts

MAKUNDI MAALUM YANUFAIKA NA ZABUNI ZA SH BILIONI 56 KUPITIA NeST

JUMLA ya zabuni 397,395 zenye thamani ya Sh40.4 trilioni zimetolewa kupitia Mfumo wa Ununuzi wa Umma Kielektroniki (NeST), huku makundi maalum yakinufaika na zabuni zenye thamani ya Sh56 bilioni tangu mfumo huo ulipoanza kutumika.

Hayo yamesemwa  Agosti 20, 2026 jijini Dodoma na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA), Dennis Simba,wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu utekelezaji wa mamlaka hiyo katika kipindi cha mwaka wa fedha 2025/26 na mwelekeo wa 2026/27.

Simba amesema matumizi ya NeST yameleta mabadiliko makubwa katika sekta ya ununuzi wa umma kwa kuongeza uwazi, ushindani, ufanisi na uwajibikaji, huku pia yakirahisisha upatikanaji wa fursa za zabuni kwa wazabuni kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Amesema takribani asilimia 70 ya bajeti ya Serikali hutumika kupitia ununuzi wa umma, jambo linaloifanya sekta hiyo kuwa eneo muhimu la fursa za biashara na utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Ukidhi wa sheria wapanda
Kwa mujibu wa Simba, matumizi ya NeST yameongeza kiwango cha uzingatiaji wa sheria katika michakato ya ununuzi wa umma kutoka asilimia 65 mwaka 2023/24 hadi asilimia 76 mwaka 2024/25 na kufikia asilimia 79 mwaka 2025/26.

Amesema mfumo huo pia umepunguza kwa kiasi kikubwa matumizi ya karatasi, ambapo zaidi ya kurasa milioni 288.57 za nyaraka za zabuni zimeepukwa kuchapishwa, hatua iliyookoa takribani Sh27.64 bilioni.

“Hivi sasa, mzabuni anaomba zabuni popote alipo,” amesema Simba, akieleza kuwa mfumo huo umeondoa ulazima wa wazabuni kusafiri kupeleka nyaraka za zabuni katika taasisi nunuzi.

Amesema hatua hiyo imepunguza gharama na muda wa wazabuni kushiriki katika michakato ya ununuzi wa umma.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!