Latest Posts

MAREKANI YAKAMATA MWANAFUNZI WA KIPALESTINA ALIYEHUSIKA NA MAANDAMANO DHIDI YA ISRAEL

Maafisa wa utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump wamemkamata Mahmoud Khalil, mwanafunzi wa Kipalestina aliyekuwa mstari wa mbele katika maandamano ya kuiunga mkono Palestina mwaka jana katika Chuo Kikuu cha Columbia jijini New York.

Kwa mujibu wa taarifa ya Chama cha Wanafunzi wa Columbia, Khalil alikamatwa Jumamosi katika makazi ya chuo kikuu na maafisa wa Wizara ya Usalama wa Ndani ya Marekani (DHS).

Kituo cha habari cha VOA kinaripoti kuwa hatua hiyo inachukuliwa kama sehemu ya juhudi za utawala wa Trump kutekeleza ahadi yake ya kuwafukuza wanafunzi wa kigeni waliokuwa wakihusika na vuguvugu la maandamano ya kuiunga mkono Palestina.

Maandamano hayo yalichochewa na shambulizi la Hamas dhidi ya Israel mnamo Oktoba 7, 2023, na operesheni ya kijeshi ya Israel iliyofuata huko Gaza, hali iliyosababisha wimbi la maandamano katika vyuo vikuu vya Marekani.

Kwa mujibu wa chama cha wanafunzi wa Columbia, Khalil ni mkazi wa kudumu wa Marekani na mke wake ni raia wa Marekani. Kufikia Jumapili, alikuwa bado anashikiliwa na maafisa wa serikali.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!