Latest Posts

MAREKANI YATHIBITISHA MAZUNGUMZO YA MOJA KWA MOJA NA HAMAS

Rais wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kile alichokiita “onyo la mwisho” kwa kundi la Hamas, akiwataka kuwaachilia mateka wote wanaoshikiliwa Gaza mara moja.

Kupitia chapisho lake kwenye mtandao wa Truth Social, Trump amesema kuwa anaitumia Israel kila inachohitaji ili kumaliza kazi na hakuna hata mwanachama mmoja wa Hamas atakayesalimika ikiwa hawatafanya kama anavyosema.

Kauli hiyo imekuja saa chache baada ya Ikulu ya Marekani kuthibitisha kuwa inafanya mazungumzo ya moja kwa moja na Hamas kuhusu mateka walioko Gaza, hatua ambayo ni kinyume na sera ya muda mrefu ya Marekani ya kutokufanya mawasiliano ya moja kwa moja na taasisi inazoziainisha kama mashirika ya kigaidi.

Katika ujumbe wake, Trump ameonya kuwa kutakuwa na athari mbaya ikiwa mateka hawataachiliwa mara moja. Hata hivyo, hakufafanua msaada wowote wa kijeshi anaoutuma kwa Israel.

Katika kauli yake kali, Trump ameongeza kuwa Hamas inapaswa kurudisha mara moja miili ya mateka waliouawa, la sivyo itakabiliwa na mashambulizi makubwa. Amewataka viongozi wa Hamas kuondoka Gaza wakati bado wana nafasi hiyo, akionya kuwa mustakabali mzuri wa watu wa Gaza hautowezekana ikiwa wataendelea kushikilia mateka. Trump amesisitiza kuwa wale wanaoshikilia mateka wamejitengenezea hatima yao mbaya.

Ikulu ya White House imethibitisha kuwa Marekani imekuwa ikifanya mazungumzo ya moja kwa moja na Hamas kwa lengo la kuhakikisha mateka wanarejeshwa salama. Msemaji wa Ikulu, Karoline Leavitt, amesema kuwa mikutano miwili ya moja kwa moja imefanyika kati ya Hamas na afisa wa Marekani Adam Boehler, ikitanguliwa na mawasiliano kadhaa. Habari hizi zimeibuliwa kwa mara ya kwanza na Axios, likisema kuwa mazungumzo yanafanyika Qatar kwa lengo la kuachiliwa kwa mateka wa Marekani pamoja na makubaliano mapana ya kumaliza vita.

Kwa mujibu wa Israel, bado kuna mateka 59 wanaoshikiliwa Gaza, huku 24 wakiaminika kuwa hai, wakiwemo raia wa Marekani. Mazungumzo haya yanaonysha uwezekano wa kufikia makubaliano ya kidiplomasia katikati ya mgogoro wa Gaza, huku Marekani ikionesha msimamo wake mkali dhidi ya Hamas.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!