Zoezi la dodoso(cross examination) kwa mashahidi watatu wa upande wa walalamikaji katika shauri la kikatiba lililofunguliwa na mawakili wa Tundu Lissu wakidai kukosa faragha ya kumuona akiwa gerezani ukonga anakoshikiliwa kwa mashtaka ya uhaini.
Kesho Julai 22, 2026 shauri hilo litaendelea kwa kuhojiwa kwa maswali ya dodoso kwa shahidi wa upande wa walalamikiwa ambaye ni Mkuu wa Gereza la Ukonga.
Baada ya shahidi wa kwanza kwa leo Wakili Nashon Nkungu ambae ni wakili wa Lissu na shahidi wa pili kwenye kesi hii Lissu alimhoji shahidi wa pili kwa leo ambaye ni Wakili Paul Kisabo ambaye ni Mkristo mwenye miaka 32.
Lissu alimtaka Wakili Kisabo kuthibitisha kuwa viapo pamoja na hati ya madai ambavyo wameapa na kusema yeye Kisabo na wenzake ni mawakili wake katika Kesi ya Uhaini iliyopo Mahakama Kuu ya Tanzania na katika kesi iliyopo Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam jambo ambalo walikubali kisha akaendelea na maswali ya dodoso.
Lissu: Waeleze majaji kuwa Bwana Jela kwenye kiapo chake kinzani amekukana kuwa hauna makubaliano ya kuwa Wakili wangu
Kisabo: Kweli
Lissu: Waeleze majaji pamoja na kukanwa umekuwa ukija mara kadhaa na kunitembelea
Kisab: Kweli
Lissu: Waeleze majaji kwamba umekuwa ukinitembelea na kuniletea fedha za chakul
Kisabo: Kweli
Lissu Waeleze majaji kwamba wiki iliyopita umenitemnelea na kuniletea fedha
Kisabo: Kweli ilikuwa tarehe 14/7
Lissu:Kwa sababu usipoleta pesa nitakosa chakula
Kisabo: Ni kweli
Lissu: Katika kiapo cha ziada cha mjibu maombi watatu ipo orodha ya mawakili ambao wanatakiwa kuniona na jina lako halipo
Kisabo:Ni kweli halipo
Lissu: Waeleze majaji kwamba pamoja na jina lako kutokuwepo lakini umekuwa ukija mara nyingi kuniona
Kisabo: Ni kweli
Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba kuna kipindi wewe pamoja na Maduhu mlizuiliwa kuniona kwa sababu majina yenu hayapo kwenye hii orodha
Kisabo: Ni kweli
Lissu: Ni kweli au si kwamba pamoja na kuzuiliwa mlishakuja kuniona mara tatu
Kisabo: Kweli
Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba Bwana Jela alikua Juma Mwaibara
Kisabo: Kweli
Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba baada ya kuzuiliwa huko mlinitumia ujumbe kupitia kwa mawakili wengine kwamba mmezuiliwa kwa sbb hampo kwenue orodha
Kisabo: Ni kweli
Lissu: Niliwatumia taarifa nimeandika orodha nyingine yenye majina
Kisabo: Kweli
Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba baada ya hapo zuio dhidi yako liliondolesa na ukaja kuniona
Kisabo: Kweli
Lissu: Licha ya kuwaambia nimeandik orodha nyingine wakili mwenzako Kulwa Maduhu alizuiiliwa
Kisabo:Kweli
Lissu: Ni kweli au si kweli kwamba tangu wakati huo hajaweza kuingia magereza
Kisabo: Kweli
Lissu: Waeleze majaji baada ya mimi kupelekewa ukonga kati ya 28, April 2025 na juni ni kweli au si kweli ilikuwa wewe na mawakili wenzako tunakutana kwenye chumba chenye kioo hatuwez kukutana uso kwa uso
Kisabo: Kweli
Lissu: Waeleze majaji kama upande wako ulikua peke yako au kinakuwa na askari magereza
Kisabo: Waheshimiwa majaji wanakuwepo na maaskari magereza wanaotusikiliza
Lissu: Kuanzia Juni mpaka Novemba utaratibu ulibadilika wewe na mawakili wenzako tulikuwa tunakutana kwenye ofisi yausajili wa wafungwa wapya ambayo ina watu wengine
Kisabo: Ni kweli
Lissu alimuelezea Kisabo mazingira ya ofisi hiyo yenye CCTV kamera huku kiti cha wakili pembeni yake kukiwa na mtu anayefanya kazi za kwenye kompyuta pakiwa na askari wawili kisha Mkuu wa Ofisi, Afisa wa sheria na askari wanaomleta Lissu huku wakiwa na uwezo wa kusikiliza yote ambayo wanaweza kuzungumza jambo ambalo alikubali.
Lissu alimhoji kisabo kama mazingira hayo yanampa Wakili nafasi ya kuzungumza na mteja wake kwa faragha jambo ambalo Kisabo alikiri hakuna mazingira.
Lissu: Novemba 15, 2025 utaratibu wa mikutano yangu na nyie mawakili wangu ulibadilika ikawa sasa badala ya kufanyia vikao kwenye ofisi ya admission sasa ikawa kwenye Ofisi ya Naibu Mkuu wa Magereza au Mkuu wa Magereza.
Kisbit:
Lissu anaeleza kuwa moja ya nyaraka aliyowahi shindwa kuipata ni Nyaraka ya jumuiya madola inayosema yeye aachiewe kwa sababu kesi inayomkabili ni ya uonevu ambapo nyaraka hiyo aliipeleka Wakili Kisabo Gereza la Ukonga lakini alipofika afisa magereza aliikataa na kumtaka wakili arudi nayo
Lissu: Ni kweli si kweli kwamba nyaraka hiyi ingeweza kunisaidia kwenye utetezi (akimaanisha katika kesi ya uhaini ambayo inamkabili)
Kisabo: Kwenye ofisi hiyo ambayo tulipelekwa alikuwa anaongoza kikao ni Afisa Magereza anaitwa Afisa Usajili wakaisoma akampa Inspekta Stima na Afisa Intelijensia akasema “Wakili hii statement rudi nayo hatuwezi kuruhusu nikasema kwa nini wakati inahusiana na kesi yake ya uhaini akasema rudi nayo.”
Kupitia maswali hayo ya dodoso aliendelea kuibua malalamiko ambapo alilalamikia kutopata wasaa wa kuongea na mawakili wake kwa usiri pindi tu anapofikishwa mahakamani wakati wa shauri la uhaini linalomkabili.
Lissu: Katika kipindi chote ambacho kesi hii ya uhaini imeendeshwa kwenye chumba hiki cha Mahakama Kuu na ni kweli au si Kweli kwamba kila siku asubuhi ninapoletwa nakwenda kufungiwa lock up.
Kisabo: Kweli
Lissu: Waeleze majaji kama kuna hata siku moja nyie mawakili wangu mmewahi kuruhusiwa kuja kuniona huko lock up
Kisabo: Waheshimiwa majaji hatujawahi kuruhusiwa.
Lissu: Waeleze majaji utaratibu unaofanyika hala ndani mahakamani wakati kesi inaendelea mkitaka kunipa nyaraka wakati kesi inaendelea inakuaje mnaruhusiwa
Kisabo: Hauruhusiwi na huwa wanazichukua hao askari magereza.(Huku akitolea mfano siku moja aliyozuiwa kumpa Lissu nyaraka mbele ya majaji)
Baada ya hapo Lissu alimtaka Kisabo kufafanua kile wanacholalamikia mahakamani kama ni kufanyia mazungumzo ofisini au lay jambo ambalo walieleza kuwa kinacholalamikiwa ni kukosekana kwa faragha wakati wa mazungumzo.
Baada ya Lissu kutamatisha maswali yake ya dodoso upande wa walalamikiwa wa kwanza mpaka wa tatu kupitia Wakili wa Serikali Mwandamizi Stanley Kalokola ulianza kuhoji maswali ya dodoso kwa shahidi Kisabo ambapo alihojiwa kama ana utaalamu wa mawasiliano kwani alisema mwanzo simu zao zilikuwa zinasikilizwa jambo ambalo Kisabo alisema yeye ana utaalamu wa sheria ambao ndani yake kuna sheria ya mawasiliano.
Aliendelea kumhoji juu ya madai kuwa maongezi yao na Lissu yamekuwa yakisikilizwa na askari magereza ambapo alimtaka kisabo kusema kama anafahamu uwezo wao kusikia ambapo alisema hafahamu lakini ni dhahiri watu hao walikuwa wanasikiliza ndio maana kuna wakati walikuwa wakiwaambia mawakili jambo hili msilizungumze.
Kalokola alihoji juu ya ukubwa wa Ofisi ya Mkuu wa Magereza jambo ambalo kisabo alieleza kuwa hajui ukubwa wake lakini kwa vipimo vya macho ni sawa na ofisi(chemba) za majaji
Kuhusu usalama wa mahabusu na wafungwa Kalokola alimhoji Kisabo kama anafahamu juu ya uwezekano wa mawakili kumdhuru mfungwa au mahabusu jambo ambalo Kisabo alisema hajui.
Wakili: Ulishasawahi kuskia mawakili ambao wanahusika na jinai
Kisabo: Sijawahi kuskia
Wakili: Unafahamu kuwa ndani ya gereza wafungwa wanaweza kudhuriana
Kisabo: Sifahamu
Wakili: Ndiyo maana utakuwa hufahamu kwa nini Mkuu wa Gereza anahusika na usalama wa wote walio gerezani.
Kisabo: Nafahamu
Baada ya hapa alimhoji Kisabo kuhusu matakwa ya kisheria au tafsiri ya kisheria juu ya faragha ambapo Kisabo alieleza kuwa sheria inataka Askari Magereza akae umbali ambao atamuona wakili na mahabusu lakini umbali huo awe hawezi kusikia kinachozungumzwa.
Upande wanalalamikaji ambao ni mawakili wa Lissu kupitia wakili wao Edson Kilatu uliweza kuuliza maswali ya kusawazisha yani Re-examination kwa Kisabo ambapo alijibu kuwa mazungumzo yao yalikuwa yanasikilizwa na Uongozi na Maafisa ea Magereza ndiyo sababu walikuwa wakiyaingilia na kuwakataza kuzungumza baadhi ya vitu.
Alimtaka pia kufafanua juu ya malalamiko waliyoleta mahakamani ambapo Kisabo alieleza wamewahi kuyawasilisha mbele ya Hakimu Mhini na Hakimu Franco Kiswaga wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakati shauri la uhaini la Lissu lilipokuwa kwenye mahakama hiyo na baadae lilipoenda mahakama kuu Lissu aliwasilisha malalamiko mara kadhaa mahakamani.
Shauri limeahirishwa litaendelea kesho Jumatano Julai 22, 2026 Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam mbele ya jopo la Majaji watatu Amir Mruma, Dkt. Angelo Rumisha na Dkt Evaristo Longopa.