Latest Posts

WAZIRI MAKONDA APUUZA UVUMI WA MAANDAMANO KUELEKEA AFCON, ‘NI MANENO YA KWENYE MABANDO TU’

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda, amepuuza taarifa na uvumi unaosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kuwepo kwa maandamano ya kuzuia michezo kuelekea Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON), akisisitiza kuwa hakuna maandamano yoyote na kwamba wananchi wanajikita katika kutafuta riziki zao halali.

Akijibu maswali ya waandishi wa habari leo, Septemba 24, 2026, jijini Dar es Salaam, Waziri Makonda ameeleza kuwa kauli hizo za maandamano ni maneno ya kimitandao yanayochangiwa na bei nafuu ya vifurushi vya intaneti. Amesisitiza kuwa mtazamo na lengo kuu la Mtanzania ni kufanya kazi kwa amani ili kujipatia kipato halali cha kuhudumia familia yake

“Nafikiri tu ni mabando tu haya yamezidi kuwa na bei nafuu wakati sisi wengine tunaona mabando ya gharama kubwa lakini wenzetu wanaona bei nafuu. Lakini Mtanzania anataka kupata kipato chake halali, anataka kutoka nyumbani asubuhi akahemea arudi nyumbani watoto wake wafanye nini? Wale”, ameeleza Makonda.

Mbali na kuzungumzia masuala ya amani kuelekea AFCON, Waziri Makonda alibainisha kuwa Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeweka miradi mikubwa mitano ya kimikakati inayofungua fursa kubwa za kiuchumi nchini

Alitolea mfano mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kusafisha mafuta (refinery) mkoani Tanga wenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 20, pamoja na mradi wa bomba la mafuta kutoka Uganda, upanuzi wa Bandari ya Tanga na Bandari ya Dar es Salaam

Waziri Makonda aliongeza kuwa kutokana na uwekezaji huo wa miundombinu, usafirishaji wa mizigo kupitia Tanga kwenda nchi jirani kama Burundi umeongezeka kutoka magari 50 hadi 100 kwa mwezi na kufikia zaidi ya malori 600 kwa siku

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!