Latest Posts

MATAPELI WA ARDHI WAIBUKIA TABORA, DC KATWALE ASHTUKIA

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wakazi wa Kidatu B katika manispaa ya Tabora mkoani Tabora wamepatwa na taharuki baada ya ndugu wawili Mohammed Nombo na Juma Nombo kudai kuwa familia zaidi ya 50 zinaishi katika eneo lao.

Eneo hilo ambalo linakadiriwa kuwa na ekari 60 ambalo ndugu Mohammed Nombo na Juma Nombo wanasema, hilo ni eneo lao ambalo waliachiwa kama shamba la urithi jambo ambalo wakazi hao wamekataa na kudai kuwa sikweli na kueleza kuwa, ndugu hao wlishindwa kesi.

Wakizungumza na wandishi wa habari wamesema, ofisi ya mkuu wa wilaya ya Tabora ilipokea hukumu mbili zinazohitaji utekelezaji wa kufanana huku kila upande ukionesha kushinda kesi hiyo ya mgogoro wa ardhi ya ekari 60 hali iliyomlazimu kumuandikia barua Jaji kutaka ufafanuzi kuhusu hukumu hizo.

Wakati akisubiri ufafanuzi wa mahakama ndipo ndugu hao wawili kutoka jijini Dar es Salam Dkt. Mohammed Nombo na Juma Nombo wakakimbilia Mahakamani wakidai mkuu huyo wa wilaya ya Tabora Katwale na kaimu Mkuu wa Polisi wilaya hiyo Selemani Mwampamba walikaidi agizo hilo.

Wakazi hao wamedai kuwa Mkuu wa Wilaya ya Tabora Deusdedith Katwale hakuzuia utekelezaji wa amri ya mahakama kama ilivyodaiwa na ndugu wawili wanaoishi jijini Dar es Salaam.

Inadaiwa, kitendo cha mkuu wa wilaya kumuandikia barua Jaji ili apate mwongozo wa utekelezaji wa hukumu hizo mbili, upande wa ndugu wawili kutoka Jijini Dar es salam haukuridhika na uamuzi huo jambo ambalo liliwafanya kumshitaki DC Katwale lakini baada ya hatua hiyo iligunduliwa kuwa hukumu waliyonayo ndugu hao wawili ni batili jambo ambalo lilimfanya mkuu huyo wa wilaya kuagiza ndugu hao wawili kutafutwa ili kuja kujibu tuhuma hizo ambapo mpaka hivi sasa vyombo vya dola vinaendelea na msako wa watu hao.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!