Latest Posts

MBUNGE MATIKO: TAA ZA BARABARANI NI MUHIMU KWA WAFANYABIASHARA WADOGO

Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mara, Ester Matiko, ameishauri Serikali kutenga bajeti maalum kwa ajili ya uwekaji wa taa katika senta zote za biashara ndani ya halmashauri za mkoa huo ili kuchochea uchumi wa wafanyabiashara wadogo na wakubwa.

Akizungumza katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika mkoani Mara, Matiko amesema kuwa uwepo wa taa barabarani na kwenye maeneo ya biashara utasaidia wananchi kufanya kazi kwa muda mrefu, hivyo kuongeza mapato yao na kukuza uchumi wa mkoa.

“Kama tunavyoona katika maeneo mengine, juzi nilikuwa nikipita Kiongela nikakuta wameweka taa, na sasa malori yanayobeba viazi yanaendelea na shughuli usiku kucha. Ikiwa serikali itatenga bajeti kwa ajili ya taa hizi, bila kujali halmashauri za miji au wilaya, senta zote zitafaidika,” amesema Matiko.

Mbunge huyo amesisitiza kuwa mkoa wa Mara una fursa kubwa za biashara na uwekezaji, lakini changamoto ya miundombinu duni ya mwanga usiku inawafanya wafanyabiashara wengi kushindwa kuendesha shughuli zao kwa muda mrefu, hivyo kupunguza fursa za kiuchumi.

Ameshauri serikali kuhakikisha bajeti inayotengwa kwa miradi ya miundombinu inajumuisha uwekaji wa taa katika maeneo muhimu, ili kusaidia wafanyabiashara na wakazi wa maeneo hayo kufanya shughuli zao kwa ufanisi zaidi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!