Latest Posts

TAMESOT YALAANI VITENDO VYA UKATILI KWA WAGANGA WA TIBA ASILI

 

Theophilida Felician Dodoma.

Chama cha waganga watiba asili nchini TAMESOT kimetoa tamko la kulaani vitendo vya ukatili ambavyo vimeanza kujitokeza kwa waganga watiba asili.

Akitoa tamko hilo kwaniaba ya chama katibu mkuu Bw Lukas Joseph Mlipu Tarehe 20 Agost 2026 akiwa Dodoma makao makuu ya TAMESOT amesema kuwa hivi karibuni wamepokea taarifa za matukio mawili yanye kusikitisha zikiwahusisha wanachama wao wawili ambao wamefanyiwa ukatili wakujeruhiwa na kuuawa.

Akiwataja waganga waliohusishwa na matukio hayo ni pamoja na Bi Bucheche Mussa mkazi wa kijiji cha Nyarutevye kata Buzuki wilaya ya Chato mkoani Gaeita yeye mnamo tarehe 15 Agost 2026 alijeruhiwa kwa mapanga na mtu ambaye hajafahamika pamoja na Mnibi Marwa Mnibi mkazi wa kitongoji cha Kwisense, kijiji Nyihara kata Kyang’ombe wilaya ya Rorya mkoani Mara anayedaiwa kuuawa na mteja wake baada ya kuondoka wote nyumbani na kuelekea porini kwa ajili ya kumpatia huduma ya matibabu baadaye kubainika akiwa ameuliwa hukohuko porini mnmo tarehe 12 Agost 2026.

Katbu mkuu Lukas amewasihi wana TAMESOT na waganga wote kwa ujumla kuchukua tahadhari katika majukumu yao ya utoaji huduma kwa jamii ili kuepukana na matukio dhidi yao huku akiwasisitiza kuendelea kusoma mafunzo yanayolenga kuwasaidia masuala mbalimbali yanayohusu kuwajengea uwezo utakaowasaidia kujitambua na kutambua mambo mbalimbali yenye kuijenga na kuiinua tiba asili.

Aidha ameliomba jeshi la polisi kuchunguza matukio hayo kwa kina ili kuwabaini wahusika waweze kuchukuliwa hatua ipasavyo.

Hatahivyo kamishina wa polisi jamii Alex Mkama akiwa ziarani mkoa wa Mara Tarehe 19 Agost amekutana na waganga watiba asili ambapo awali ametoa pole kwa familia ya wana TAMESOT kufuatia matukio hayo yakikatili kwa wenzao huku akisisitiza uchunguzi ufanyike ili kuwabaini wahalifu waliohusika na matukio hayo waweze kufikishwa kwenye vyombo vya sheria.

Kamishina Alex pia ametoa wito kwa waganga kuzingatia masuala muhimu hususani kuwatambua wageni wanaowapokea kwa ajili ya kuwahudumia tiba kwa kuwataka utambulisho wao hata wanapokwenda kutoa huduma porini wawe na wasaidizi badala ya kwenda na mteja pekee.

Mbali na hayo ametoa wito akiwaonya wanaotoa huduma bila kufuata misingi ya tiba asili kwa lengo la kupiga ramli chonganishi, utapeli na mengineyo kuacha mara moja kwani atakayebainika atachukuliwa hatua kali za kisheria.

Amehitimisha akiwasihi waganga kufanya kazi kwa weledi sambamba na kupata mafunzo maalumu kwao yanayotolewa na TAMESOT kwa kushirikiana na mamlaka nyingine za serikali huku akiahidi jeshi la polisi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuzishughulikia changamoto zao kiusalama kama ilivyo kwa jamii nzima.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!