Latest Posts

MBUNGE NJEZA AKABIDHI MIZINGA YA NYUKI, ‘ILANI IMEENDA VIZURI’.

Na Josea Sinkala, Mbeya.

Katika kutekeleza kwa vitendo dhana ya Siasa na uchumi ndani ya Chama Cha Mapinduzi CCM, Mbunge wa jimbo la Mbeya vijijini Mhe. Oran Manasse Njeza, amekabidhi mizinga kumi ya nyuki kwa jumuiya ya wazazi wa CCM Wilaya ya Mbeya vijijini ili kujiimarisha kiuchumi na kuendelea kuijenga jumuiya na Chama hicho hasa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa kutokuwa na uchumi tegemezi.

Akizungumza kwenye kikao na viongozi wa jumuiya ya wazazi kutoka kata mbalimbali za chama hicho, Mbunge wa Mbeya vijijini ameeleza umuhimu wa Chama kujisimamia kiuchumi na kuendelea kujiandaa na uchaguzi mkuu wa mwaka huu kwa kuhakikisha viongozi na wanachama wanaimarisha jumuiya zao na chama ili kwenda kushinda kwa kishindo uchaguzi huo kutokana na utekelezwaji mzuri wa ilani yao (CCM) akisema huu ni wakati wa kuendelea kueleza utekelezwaji wa miradi uliofanyika na unaoendelea kufanyika katika maeneo mbalimbali.

 

Amebainisha miradi mbalimbali ambayo imetekelezwa ikiwemo katika jimbo lake hasa uboreshaji wa idara ya afya kwa ujumla, ujenzi wa vyumba vya madarasa, ujenzi wa barabara kwa viwango tofauti na kufanya kupitika tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma sanjari na nishati ya umeme ambayo imefikishwa katika vijijini vyote na kwamba sasa Serikali imeanza kusambaza nishati hiyo kwenye vitongoji.

Kwa upande wake afisa nyuki wilaya ya Mbeya Gerald Shayo, amewataka viongozi na wananchi wilayani Mbeya kuzingatia uhifadhi bora wa mazingira ili kutunza uoto wa asili.

Shayo amesema pia ikiwa wananchi watatilia maanani ufugaji wa nyuki watapata faida ikiwa ni pamoja na kwa jumuiya ya wazazi ambayo ina mradi wa ufugaji wa nyuki wilayani humo kutokana na faida mbalimbali zitokanazo na ufugaji huo ikiwemo kuinua uchumi kwani asali zina soko la uhakika pamoja na kula mazao ya nyuki kwa faida yao kiafya.

Viongozi na wanachama mbalimbali akiwemo mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi wilaya ya Mbeya Mwalimu Willium Simwali, wamemshukuru Mhe. Mbunge wa Mbeya vijijini kwa kutekeleza ahadi yake aliyoitoa Februari 22, 2025 mbele ya mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi Taifa kuwa atachangia mizinga kumi ya nyuki kwa jumuiya hiyo wilaya ili kuendeleza mradi wao wa ufugaji nyuki.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!