Baadhi ya wananchi wa Jimbo Jipya la Chato Kusini, mkoani Geita, wameibua kilio chao wakimtaka kwa nguvu zote kurejeshwa katika orodha ya wagombea wa ubunge mtia nia Paschal Lutandula, wakieleza kuwa ndiye chaguo sahihi linalojua na kuelewa shida zao.
Wakizungumza kwa hisia kali, wananchi hao wamesisitiza kuwa wanahitaji kiongozi anayewatoka wao, ambaye ana uelewa wa moja kwa moja juu ya changamoto zinazowakabili, na hivyo kuwa na nafasi nzuri ya kuzitatua kwa haraka na kwa ufanisi.
Kwa upande wake, mtia nia wa nafasi ya Ubunge katika jimbo hilo, Paschal Lutandula, ameahidi kuwa endapo atapewa ridhaa na wananchi, atakuwa mtumishi mwaminifu na mwakilishi wa kweli wa wananchi Bungeni.
Jimbo la Chato Kusini ni miongoni mwa majimbo mapya yaliyoundwa hivi karibuni, na tayari limekuwa kitovu cha hamasa ya kisiasa huku wananchi wakionyesha ushawishi mkubwa wa kutaka wawakilishi wanaowajua kwa karibu.