Latest Posts

MIKAKATI YA RAIS SAMIA, TANZANIA KUWA NAMBA MOJA UZALISHAJI WA CHAKULA AFRIKA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweka wazi malengo ya Serikali ya Tanzania ya kuifanya nchi kuwa mzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika, akibainisha mikakati mitatu mikuu katika sekta ya kilimo.

Akizungumza nchini Marekani mnamo Oktoba 30, 2024, wakati wa mjadala wa kilimo barani Afrika uliofanyika katika mji wa Des Moines, Iowa. Mjadali huo uliandaliwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) na kuwaleta pamoja viongozi mbalimbali kutoka mataifa ya Afrika, pamoja na wawakilishi kutoka serikali ya Marekani na sekta binafsi, hasa wale wanaohusika na kilimo. Lengo la mjadala huo lilikuwa kushughulikia changamoto za kilimo zinazokabili Afrika na kuchunguza njia za kushirikiana kati ya mataifa ya Afrika na wadau wa Marekani kwa ajili ya suluhisho

Rais Samia ameelezea jinsi serikali ya Tanzania inavyolenga kuimarisha sekta hiyo kwa hatua madhubuti za uwekezaji na ushirikiano na wadau wa maendeleo.

Kwa mujibu wa Rais Samia, mkakati wa kwanza ni kuwekeza katika miundombinu ya umwagiliaji ili kuimarisha uwezo wa uzalishaji wa mazao kwa mwaka mzima, hali inayopunguza utegemezi wa mvua na kuongeza mavuno. Mkakati huu unalenga kuhakikisha ardhi nyingi zaidi inatumika kuzalisha mazao ya chakula kwa ufanisi mkubwa, hatua inayotarajiwa kuleta ongezeko kubwa la uzalishaji.

Katika hotuba yake, Rais Samia amebainisha kuwa Afrika ina uwezo mkubwa wa kilimo ambao bado haujatumiwa ipasavyo. “Kwa uwekezaji na ushirikiano sahihi, tunaweza kubadilisha sekta ya kilimo ili sio tu kuwalisha watu wetu, bali pia kuchangia kwa kiasi kikubwa kwenye upatikanaji wa chakula duniani,” amesema.

Pia, Rais Samia ameeleza kuwa Serikali imejikita katika kuboresha upatikanaji wa teknolojia na pembejeo za kisasa kwa wakulima, hatua inayotazamiwa kuongeza tija na ubora wa mazao. Amesema kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, Serikali inaendelea kutoa mbinu na vifaa vya kisasa kwa wakulima, jambo ambalo litawawezesha kupata mazao yenye thamani kubwa katika masoko ya ndani na kimataifa.

Aidha, Rais Samia ameelezea mkakati wa kukuza masoko ya mazao ya kilimo nchini kwa kuhakikisha kuwa mazao yote yanayozalishwa yanapata masoko ya uhakika ndani na nje ya nchi. Mpango huu una lengo la kuwapa wakulima fursa zaidi za kuuza mazao yao na kupata faida kubwa zaidi kutokana na kazi zao, hatua inayosaidia kuinua kipato chao na kuchangia uchumi wa taifa.

Kwa kuzingatia mikakati hii mitatu, Rais Samia amebainisha kuwa Tanzania inatarajiwa kuwa mzalishaji mkuu wa chakula barani Afrika, hivyo kuchangia katika usalama wa chakula kwa kanda nzima na kuimarisha nafasi ya nchi katika soko la kikanda na kimataifa.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!