Latest Posts

MVUA KUBWA MTWARA YASABABISHA ATHARI KWA WANAFUNZI WA VYUO VIKUU

Kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha mkoani Mtwara na kusababisha athari kwa baadhi ya maeneo hususani kwa wanafunzi 35 wanaosoma Chuo Kikuu cha Stella Maris STEMUCO na Chuo cha Utumishi Wa Umma Mtwara vilivyopo kwenye Manispaa ya Mtwara Mikindani.

Wanafunzi hao 35 kutoka kwenye vyuo hivyo ambao wameathiriwa na mvua kwenye hostel wanayoishi ya Prorata iliyopo kata ya Shangani, Mtaa wa Kiyangu ‘B’ kwenye manispaa hiyo wamekabidhiwa Shilingi 300,000 ikiwa ni mkono wa pole kwa wanafunzi hao.

Aidha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya amesema fedha hiyo iliyotolewa ni ya awali ambayo itawasaidia kununua chakula wakati serikali ikiendelea kufanya jitihada zingine.

Pia Mwaipaya amewataka wanafunzi hao kuendelea kuchukua tahadhari kwa kuwa mvua bado zinaendelea kunyesha na kuwasisitiza kusoma kwa bidii huku akiwataka kuwasiliana na viongozi inapotokea wamepata changamoto yoyote.

Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara, Mikindani Sixmund Lungu amesema kuwa Manispaa itashirikiana na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Mtwara katika kuweka mikakati ya kuimarisha miundombinu ya barabara na mifereji ili kupunguza athari zitokanazo na mvua.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Emmanuel Zengo, Rais wa Serikali ya wanafunzi wa Chuo cha STEMUCO Mtwara ameishukuru Serikali kwa msaada waliotoa kwa wanafunzi hao na ameiomba kuendelea kuwashika mkono kwa kuwa wanafunzi hao kwa sasa wana mahitaji mengi kama vile chakula, madaftari, taulo za kike na mahitaji mengine.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!