Latest Posts

MWENYEKITI BAVICHA SHINYANGA MJINI MATATANI TUHUMA ZA KUHAMASISHA MAANDAMANO

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limethibitisha kumkamata Mwenyekiti wa Baraza la Vijana wa Chadema (BAVICHA) Wilaya ya Shinyanga, Bw. Alfred Masanja (43), mkazi wa Ndala, kwa tuhuma za kuhamasisha maandamano yaliyokuwa yamepangwa kufanyika Julai 7, 2026.

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa Julai 17, 2026, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Janeth Magomi, amesema Masanja anadaiwa kuwahamasisha vijana kutoka makundi mbalimbali kushiriki katika maandamano katika maeneo tofauti ndani ya Mkoa wa Shinyanga.

Kamanda Magomi amesema uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa huyo unaendelea na kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa baada ya kukamilika kwa uchunguzi.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linaendelea na mahojiano na uchunguzi dhidi ya mtuhumiwa huyo, baada ya kukamilika kwa uchunguzi taratibu stahiki zitachukuliwa kwa mujibu wa sheria za nchi.” amesema SACP Janeth Magomi.

Katika onyo lake kwa umma kuhusu masuala ya usalama, Kamanda Magomi amesisitiza kuwa Jeshi la Polisi Mkoani humo halitavumilia vitendo vinavyoweza kuvuruga amani.

“Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linatoa wito kwa wananchi kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani kwani halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayejaribu kuvuruga amani.” amesema.

Jeshi la Polisi Mkoani Shinyanga kadhalika limewataka wananchi kuendelea kuheshimu sheria za Nchi na kushirikiana na vyombo vya dola katika kulinda amani na usalama wa Mkoa wa Shinyanga.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!