Latest Posts

NAIBU WAZIRI SANGU AELEKEZA HALMASHAURI KUTOA MIKOPO KWA VIKUNDI VYA TASAF

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Deus Sangu amezielekeza halmashauri za mkoa wa Tabora kutoa kipaumbele kwa vikundi vya akiba na mikopo vinavyoundwa na walengwa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) katika utoaji wa mikopo.

Akizungumza wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi ya TASAF katika Kata ya Ipuli, wilayani Tabora, Sangu amesema kuwa vikundi hivyo vimepatiwa elimu ya ujasiriamali na nidhamu katika ukopaji, hivyo vinastahili kupewa mikopo.

“Vikundi hivi vinaonesha uwezo mkubwa wa kujipanga kiuchumi kupitia TASAF, na kwa sababu hiyo, vinapaswa kupewa kipaumbele na halmashauri katika utoaji wa mikopo,” amesema Sangu.

Amesisitiza kuwa mikopo ya asilimia kumi inayotolewa na halmashauri inapaswa kushirikiana na TASAF ili kujifunza kutoka mafanikio ya vikundi hivyo katika kuweka akiba na kukopeshana.

Aidha, Sangu ameeleza kuwa mpango wa ajira za muda unaotekelezwa na TASAF siyo tu unalenga kutoa ajira za muda kwa walengwa, bali pia unawasaidia kujifunza ujasiriamali na ufundi unaowawezesha kujikwamua kiuchumi. Hata hivyo, amesisitiza kuwa makundi kama wazee wenye zaidi ya miaka 65, watoto chini ya miaka 18, wanawake wajawazito, na watu wenye ulemavu hawapaswi kushiriki katika kazi hizo.

Sangu pia ameagiza kaya za walengwa zenye vijana waliohitimu Kidato cha Sita kuwasiliana na TASAF ili wapatiwe barua za kuambatanisha na maombi ya mkopo kwa ajili ya masomo ya elimu ya juu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Paul Chacha ameeleza kuwa ujio wa TASAF umewasaidia sana wananchi wa mkoa huo, huku wanufaika zaidi ya 13,000 wakijiunga na bima ya afya iliyoboreshwa (CHF), kuboresha makazi yao, na kuanzisha vikundi vya kukopeshana.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!