Latest Posts

PBPA YASHIRIKI MDAHALO WA NISHATI SAFI ZANZIBAR

Meneja wa Mipango ya Mafuta wa Wakala wa Uagizaji Mafuta kwa Pamoja (PBPA), Bw. Gilbert Jungulu, amemuwakilisha Mtendaji Mkuu wa PBPA kushiriki katika Mdahalo wa Nishati Safi uliofanyika leo, Agosti 11, 2026, katika Hoteli ya Kwanza, Kizimkazi, Mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

Mgeni rasmi katika mdahalo huo alikuwa Waziri wa Nishati, Mhe. Deogratius Ndejembi (Mb.), ambaye ameongoza viongozi na wadau mbalimbali kutoka Tanzania Bara na Zanzibar katika kujadili masuala yanayohusu matumizi na maendeleo ya nishati safi nchini.

Waziri Ndejembi ameambatana na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba (Mb.), Katibu Mkuu (Umeme na Nishati Jadidifu), Mhandisi Felchesmi Mramba, pamoja na Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Nishati.

Mdahalo huo umeandaliwa na Mwanamke Initiative Foundation, chini ya uongozi wa Mwenyekiti wake, Mhe. Wanu Hafidh Ameir, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia.

Ushiriki wa PBPA katika mdahalo huo ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali za kuhamasisha matumizi ya nishati safi na kuchochea ushiriki wa wadau katika kufanikisha ajenda ya Taifa ya mpito kuelekea matumizi ya nishati safi na endelevu.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!