Latest Posts

POLISI KATA IKOMA AVISHWA CHEO CHA SAJENTI KUTOKANA NA UTENDAJI KAZI WAKE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Pius Lutumo kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Polisi Inspekta Jenerali wa Polisi Camilius Wambura amemvisha cheo cha Sajenti Polisi kata wa kata ya Ikoma Wilayani Serengeti, mkoani Mara Koplo Emmanuel Kisiri kutokana na jitihada alizozionesha katika utendaji wa kazi katika kata yake kwa kushirikiana na kujiweka karibu zaidi na jamii anayoihudumia pamoja na wadau mbalimbali.

Hafla fupi ilifanyika katika kiwanja cha kikosi cha kutuliza ghasia Kamnyonge Manispaa ya Musoma mkoani Mara na kuhudhuriwa na maofisa wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali wa mkoani humo.

Baada ya kumvisha cheo hicho, Kamanda Lutumo alipata wasaa wa kuzungumza na askari hao ambapo amewataka kufanya kazi kwa uadilifu kila wakati kutokana na mafunzo waliyoyapata katika kuwahudumia wananchi.

“Kutokana na jitihada alizozionesha Koplo Emmanuel Kisiri ni dhahiri kuwa ana uwezo wa kuongoza hivyo anastahili kutunukiwa cheo cha Sajenti”, amesema Kamanda Lutumo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!