Latest Posts

PPRA MTWARA YAOMBWA KUTOA FURSA YA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya ameitaka Mamlaka ya Udhibiti na Ununuzi wa Umma PPRA Mkoa wa Mtwara kutoa fursa ya elimu kwa wafanyabiashara juu ya ufanyaji biashara na serikali kupitia miradi ya maendeleo inayotekelezwa kwa fedha ambayo itawainua kiuchumi.

Ameyaeleza hayo Februari 28, 2025 wakati wa uzinduzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma Kanda ya kusini, hafla iliyofanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani ulioambatana na ufunguzi wa mafunzo kwa waandishi wa habari yenye lengo la kuwajengea uwelewa zaidi wanahabari hao juu ya suala zima la mfumo wa usimamizi wa ununuzi wa umma.

Amesema kuwa Mtwara na maeneo mengine wapo wafanyabiashara wengi ambao wanatamani kufanya baishara lakini hawajui au kufahamu namna ya kufanya biashara na serikali

“Sekta ya ununuzi wa umma maarufu kama Tenda za serikali inafursa zinazotokana na zaidi ya asilimia 70 ya bajeti kuu ya serikali na fursa hiyo inapatikana kwa njia ya kufanya biashara na serikali hivyo ni jukumu letu sisi kuwafahamisha kwamba kuna ppra wao wanayo nafasi kubwa ya kuwaelekeza wafanyabiashara katika mkoa wetu kuwa kwa namna gani wanaweza kufanya biashara na serikali.”Amesema Mwaipaya

Pia Wilaya ya Mtwara ni miongoni mwa wilaya za kanda ya kusini ambazo zina fursa nyingi za kiuchumi kwa sekta mbalimbali na wananchi wenye nguvu na nia ya kuchangia kwenye maendeleo ya Taifa.

Ameongeza kuwa mkoa wa Mtwara una miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na fedha za serikali ambapo miradi hiyo yote inategemea wafanyabiashara kwaajili ya kusambaza nyenzo mbalimbali za kazi.

Kaimu Meneja wa PPRA Kanda ya Kusini Fenias Manasse amesema kazi kubwa ya kitengo hicho ni kuhakikisha mfumo wa ununuzi nchini unafuata sheria, kanuni,taratibu na kuakisi thamani ya fedha katika michakato yote ambayo inafanyika ili serikali iweze kupata ela ambayo imekusudia.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari mkoani Mtwara Grace Kasembe, kwa niaba ya waandishi ameishukuru PPRA kwa kutambua mchango wa waandishi na kuona umuhimu wa kuwapatia elimu  hiyo na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa kuhabarisha umma kuhusu elimu hiyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!