Latest Posts

RC CHALAMILA AKUTANA NA KAMATI YA BUNGE YA ARDHI MALIASILI NA UTALII

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila Jumatatu Julai mosi, 2024 amekutana na Kamati ya Bunge ya Ardhi Maliasili na Utalii katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo Ilala Boma.

Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti wake Timotheo Paul Mnzava iko katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Dar es Salaam ambapo Jumapili Juni 30, 2024 ilitembelea miradi ya NHC Kawe na Morocco Square na Julai mosi 2024 imeendelea na ziara Gongo la Mboto Ilala kukagua maendeleo ya mradi wa ukwamuaji wa zoezi la urasimishaji wa ardhi.

Akiongea na kamati hiyo RC Chalamila ameipongeza kwa namna inavyotekeleza majukumu yake na kufanya ziara katika mkoa huo ambapo amesema mkoa huo bado una changamoto ya  migogoro ya ardhi na ofisi yake inaendelea kutatua migorogoro hiyo.

Pia amezungumzia suala la maji kujaa nyakati za mvua ambapo amesema yeye hawezi kuita ni mafuriko kwa sababu sehemu nyingi zinazojaa maji ni zile ambazo zimejengwa kiholela na kuzibwa kwa mifereji ya maji hivyo ni vema upimaji na upangaji wa miji uakisi changamoto hiyo.

Aidha kwa upande wa mwenyekiti wa kamati Mnzava amesema ni wakati muafaka wa kuwekeza katika urasimishaji kwa kuwa tayari makosa yalishafanyika hivyo urasimishaji ni kujisahisha.

Pia amesema kwa mkoa wa Dar es Salaam katika utalii ni lazima kuweka mikakati ya makusudi kwenye utalii wa fukwe na hoteli kwa kuwa wageni wengi hutembelea mkoa huo wa kibiashara.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!