Latest Posts

RC MAKONDA: ‘KARIBU KILI FAIR 2024’ KUCHOCHEA UTALII WA ARUSHA

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Makonda amesema maonesho ya Karibu Kili Fair 2024 yanayotarajiwa kuanza Juni 7 yatachochea na kusisimua utalii wa Arusha kwa kiasi kikubwa, akiwataka wananchi na wadau wa utalii kuchangamkia fursa ya uwepo wa maonesho hayo.

RC Makonda ametoa kauli hiyo Jumatano Juni 5, 2024 mara baada ya kukagua maandalizi ya maonesho hayo yatakayofanyika kwenye viwanja vya Magereza Arusha na kufunguliwa na Waziri wa Maliasili na utalii Angellah Kairuki.

Maonesho hayo yanatarajiwa kushirikisha kampuni za kimataifa zaidi ya 700 kutoka mataifa takribani 50 na kampuni wenyeji zaidi ya 500 zitakazoonesha bidhaa na kazi mbalimbali.

Makonda amewataka wadau wa utalii kushiriki kikamilifu kwenye maonesho hayo ili kutangaza huduma zao pamoja na kubadilishana uzoefu na kampuni zingine ili kusaidia kukuza utalii Arusha.

Kadhalika Makonda amewakaribisha wananchi na raia wote wa kigeni kwenye maonesho hayo akiwahakikishia ulinzi na usalama kwa muda wote wa maonesho yatakayofanyika kwa siku tatu mtawalia kuanzia Juni  07.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Kili Fair, Dominic Shoo amemuambia Mkuu wa Mkoa kuwa maandalizi yamekamilika kwa asilimia 95 akisisitiza kuwa maonesho ya mwaka huu yameboreshwa zaidi ikiwamo kuongeza saa za maonesho na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya michezo ya watoto.

Maonesho ya Karibu Kili Fair 2024 yanafanyika kwa awamu ya tisa Jijini Arusha, likiwa ni jukwaa maalumu la kuweka pamoja kampuni za ndani na nje ya nchi zinazohusika na sekta ya utalii ili kubadilishana bidhaa, huduma na uzoefu unaotokana na sekta ya utalii duniani.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!