Latest Posts

RC MALIMA: PATO LA LINDI LAPANDA HADI TRILIONI 4.6

Mkuu wa Mkoa wa Lindi Adam Malima, amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya CCM Mkoa wa Lindi kwa kipindi kuanzia Julai 2025 hadi Juni 2026 kwenye kikao cha Halmashauri kuu ya CCM Mkoa wa Lindi.

Taarifa hiyo imeangazia katika sekta zote tambuka zinazogusa jamii moja kwa moja kama vile huduma ya afya ambapo Mkoa wa Lindi una vituo vya kutolea huduma za afya 331, kati yake zipo Hospitali 11 (Serikali 9, zisizo za Serikali 2), Vituo vya Afya 39 (Serikali 38, visivyo vya Serikali 1), Zahanati 282 (Serikali 264, zisizo za Serikali 18) na Kliniki 1 ya binafsi.

Kwa upande wa elimu, Malima amesema, katika kipindi cha Julai 2025 hadi Juni 2026, Serikali imetoa Bilioni 19.15 kati ya hizo Bilioni 11.536 zimetumika katika kuinua na kuboresha miundombinu sanjari na mazingira ya kujifunza na kufundishia. Sekta ya maji, hali ya upatikanaji wa huduma ya maji safi katika mkoa imefikia 74%. Kwa Mwaka wa Fedha 2025/26 Sekta ya Maji mkoa umepewa bilioni 25 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji.

Ilani imetekelezwa katika kuhakikisha barabara zinapitika wakati wote ingawa yapo maeneo ambayo bado changamoto ya barabara kupitika wakati wote ipo. Katika kutatua hilo Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mkoa wa Lindi unasimamia Mtandao wa barabara wenye jumla ya urefu wa kilometa 4,803.50. Mtandao huo umegawanyika katika sehemu kuu tatu kama ifuatavyo; barabara za Wilaya 2,503.058 km sawa na 52.11%,

Kwa ujumla hali ya uchumi wa mkoa wa Lindi imeendelea kuimarika kutoka trilioni 4.1 hadi trilioni 4.6 kwa mwaka 2025.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!