Latest Posts

TABOA: MGOMO UMEKWISHA, ABIRIA JITOKEZENI KUSAFIRI

Chama cha Wamiliki wa Mabasi Tanzania (TABOA) kimetangaza kumalizika kwa mgomo wa madereva wa mabasi ya masafa marefu na kuwataka abiria kujitokeza kusafiri kurejea kwenye shughuli zao, huku kikiisistiza Serikali kuzingatia na kuzifanyia kazi kwa dhati hoja za msingi za madereva ili kuzuia kujirudia kwa migogoro hiyo.

Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa TABOA, Mustafa Mwalongo, ameyasema hayo leo tarehe 30 Septemba 2026 alipokuwa akizungumza na wanahabari katika Kituo Kikuu cha Mabasi cha Magufuli (Mbezi) jijini Dar es Salaam, ikiwa ni siku moja tangu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, alipokutana na kuzungumza na madereva na abiria jioni ya tarehe 29 Septemba 2026 kufuatia mgomo huo.

Hata hivyo, Mwalongo ameeleza kuwa baada ya Waziri kuondoka jana, kundi la madereva halikukubaliana na majibu hayo na lilitaka mgomo uendelee. Mzozo huo uliwalazimu viongozi wa TABOA kukutana saa 5:00 usiku na kuanza kupiga simu kwa wamiliki wa mabasi ili wazungumze na madereva wao.

“Magufuli tuna idadi ya magari yanayotoka kwa siku yasiyopungua 400… time table nyingi watu wanachukua jioni kuanzia alasiri kwa maana ya saa 9:00, saa 10, 11 usiku wa saa 2:00, saa 3:00, saa 4:00 hapa ndio tunakuwa tuna ‘peak kubwa’ ya magari yanayoondoka. Hivyo tunatarajia leo hizo gari 400 zitaondoka na abiria wengi watasafiri. Kwa hiyo naomba niwatangazie abiria kwamba mgomo umekwisha.”, ameeleza.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!