Latest Posts

TAKUKURU MTWARA YAOKOA ZAIDI YA SHILINGI MILIONI 79 ZA WAKULIMA WA KOROSHO

Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa Mtwara, imesaidia kufanikisha kupatikana kwa malipo ya wakulima wa Korosho msimu 2024/2025 ambayo yalikuwa yamekwamishwa na viongozi wa vyama vya msingi vya ushirika.

Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TAKUKURU tarehe 27 Mei 2025, Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Mtwara Elisante Mashauri, ameeleza kuwa kiasi cha fedha shilingi 79,837,568 ambazo ni fedha za wakulima wa korosho walizokuwa wanadai katika msimu 2024/2025 zililipwa katika kipindi cha Januari hadi machi 2025.

Katika hatua nyingine TAKUKURU Mkoa wa Mtwara imefanya ufuatiliaji wa rasilimali za umma kwa kukagua miradi ya maendeleo 13 yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 7 katika sekta ya Afya, Miundombinu na Elimu ili kubaini viashiria vinavyoweza kusababisha upotevu wa fedha za umma.

Miradi hiyo ni Ujenzi wa shule ya sekondari Mtunguru uliopo Halmashauri ya Wilaya ya Newala ambao ulikuwa na thamani ya shilingi milioni 560,552,827.00 ambapo ufuatiliaji ulibaini mpango kazi kukosa uhalisia na kasi ndogo ya utekelezaji.

Pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kuu Masasi _Nanyumbu kwenye kipande kilichokuwa kinafanyiwa ukarabati kwa thamani ya shilingi milioni 705,550,000.00 na kubaini uwepo wa kifusi kilichotolewa kwenye chanzo tofauti na kilichokuwa kimependekezwa bila kufanyiwa majaribio hivyo takukuru ilishauri na kifusi hicho kilifanyiwa majaribio na kutolewa majibu kuwa kinafaa.

Pia Mashauri amesema wataendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu umuhimu wa kushiriki katika uchaguzi mkuu,sifa za kiongozi anayestahili kuchaguliwa na madhara ya rushwa kwenye uchaguzi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!