Latest Posts

TCB NA ZEEA ZASAINI (MOU) KUSAIDIA WAFANYABIASHARA WADOGO ZANZIBAR

LBenki ya Biashara Tanzania (TCB) Agosti Mosi, 2024 imesaini mkataba wa makubaliano (MOU) na Wakala wa Serikali wa Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi Zanzibar ( ZEEA), Makubaliano haya ya kimkakati ambayo yanalenga kuanzisha mpango maalum wa mikopo utakaonufaisha makundi maalumu wakiwemo wanawake na vijana wenye ulemavu wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi Visiwani Zanzibar. Mpango ambao unakusudia kuchochea ukuaji wa biashara, ongezeko la ajira, na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Akizungumza na waandishi wa Habari Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Adam Mihayo amesema Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla na kwamba Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha
uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.

Amesema Mkataba huo utawezesha kutoa mikopo nafuu kwa makundi kwa kiasi cha shilingi milioni 30 kwa kikundi, huku wakipewa muda miezi 24 sawa na
miaka miwili Kwa kutoa mikopo nafuu kwa makundi hayo, TCB na ZEEA watawasaidia wajasiriamali kupanua biashara zao, kutengeneza fursa mpya za ajira, na hivyo kupunguza uhaba wa ajira.

Mpango huu pia utazisaidia biashara kujiendesha, kukabiliana na mfumuko wa bei, pamoja na kuwekeza katika vitendea kazi, na kuzipa ustahimilivu,Tuna furaha kushirikiana na ZEEA kuwainua wajasiriamali wanawake, vijana na makundi mengine maalum yaliyomo visiwani Zanzibar,” alisema Mihayo

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA Juma Burhani Mohamed amesema wanalenga kuipatia benki ya TCB kiasi cha shilingi bilioni 1.8 ili waanze utoaji wa mikopo hiyo na kwamba Mpango huu unaendana na lengo la kuwezesha maendeleo ya kiuchumi kwa kujenga uchumi jumuishi Kwa kuyawezesha makundi maalum, wanaziinua biashara binafsi, pamoja na kuimarisha mfumo mzima wa uchumi na kutengeneza mazingira imara ya
kiuchumi.” alisema

Mbali na kuchangia maendeleo ya kiuchumi, makubaliano haya pia yanakusudia kuimarisha uchumi wa buluu visiwani Zanzibar. Kupitia mikopo hii itakayoinua biashara ndani katika sekta hii, TCB na ZEEA wanapigia chapuo eneo hili nyeti la
shughuli za kiuchumi lenye uwezo wa kuchangia maendeleo kwa kiasi kikubwa.

Mchango wa Benki ya TCB katika kuunga mkono jitihada za Serikali katik na kupokea maombi ya mkopo yanayofikia wastani wa Mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali, kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha biashara na uchumi.

Akishuhudia kusainiwa kwa hati hizo jijini Dar es salaam Katibu mkuu ofisi ya Rais Kazi Uchumi na Uwekezaji Zanzibar Mariam Juma Abdullah amesema tayari shilingi bilioni 2 zimeshakusanywa na halmashauri visiwani humo ili kuanza uwezeshaji akiitaka benki ya TCB kuhakikisha inafanya tathmini ya mikopo wanayotoa kwa makundi hayo ili ziweze kurejeshwa kwa wakati na wengine waweze kukopa .

Ameeleza kuwa mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali, kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao.

Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha
uchumi wa ndani, kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupambana na ukosefu wa ajira na kuleta maendeleo na kuwa Kupata fursa ya mikopo ni muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa biashara ndogondogo na za kati.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!