Latest Posts

TEA YASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA MASHUJAA, WAKITAMBUA MCHANGO WAO KATIKA KUPIGANIA UHURU


Tanzania huadhimisha Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda uhuru wa Tanzania kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka.

Siku hii ya kuwakumbuka mashujaa huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalum ya kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi kutoka kwa viongozi wa dini.

Leo Julai 25, 2024 Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imeshiriki kuadhimisha kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika Mtumba jijini Dodoma kuungana na Watanzania wote kutambua mchango wa Mashujaa hao katika kuupigania Uhuru wa Tanzania.

Katika maadhimisho hayo, viongozi mbalimbali wa serikali, dini na wakuu wa taasisi walihudhuria ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!