Latest Posts

TEF YAWAPONGEZA WALIOTEULIWA KUUNDA BODI YA ITHIBATI YA WANAHABARI

 

Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) limetoa pongezi kwa Mwenyekiti wa Bodi, Tido Mhando na Wajumbe Ndugu Thobias Makoba, Ndugu Kingoba Mgaya, Dkt. Rose Reuben, Dkt. Egbert Mkoko, na Ndugu Ladislaus Komanya kwa kuteuliwa kuunda wajumbe wa Bodi ya Ithibati ya Wanahabari.

Pongezi hizo pia zimeelekezwa kwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Jerry William Slaa aliyefanya uteuzi huu Septemba 18, 2024 na kukamilisha kazi iliyokwamisha utekelezaji wa sheria hii tangu mwaka 2016, yaani miaka minane iliyopita. Uteuzi huu ulioanza Septemba 18, 2024 utadumu kwa kipindi cha miaka mitatu.

TEF inatumaini kuwa, kuteuliwa kwa Bodi ya Ithibati, kutaanzisha mchakato wa kuundwa kwa Baraza Huru la Habari Tanzania (IMCT), ambalo sasa linakwenda kumaliza tatizo sugu la makosa ya kitaaluma kwa wanahabari kupelekwa mahakamani tofauti na taaluma nyingine nchini.

“Tunaamini Mwenyekiti na wajumbe walioteuliwa wataifanya kazi hii kwa weledi mkubwa na kwa masilahi ya kukuza taaluma hasa katika kipindi hiki ambacho vyombo vya habari vina changamoto kubwa ya uchumi.T unawatakia kila la heri na kuwaombea katika kazi hii ambayo taaluma ya habari sasa inawekeza matumaini yote kwao” Imeeleza sehemhu ya taarifa kwa umma iliyotolewa na na kusainiwa na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), Deodatus Balile

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!