Latest Posts

TEKNOLOJIA KUTUMIKA WAKATI WA EL NIÑO KUTOA HAKI KWA WAKATI

Waziri wa Katiba na Sheria, Abdallah Hamis Ulega amefanya ziara yake ya kwanza ya kujitambulisha katika Makao Makuu ya Mahakama ya Tanzania jijini Dodoma, ambapo alikutana na Jaji Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, George Masaju, kufuatia uteuzi wake wa hivi karibuni uliofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Katika mazungumzo hayo ya Oktoba 12, 2026 yaliyohudhuriwa pia na Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Dkt. John Jingu, pamoja na viongozi wengine wa Mahakama, Waziri Ulega ameomba ushirikiano thabiti katika utekelezaji wa majukumu ya sekta ya haki nchini. Sambamba na hilo, ameonesha kuvutiwa kwake na kuipongeza Mahakama kwa kuwa na miundombinu bora ya majengo, uwekezaji mkubwa katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA), pamoja na maandalizi madhubuti yaliyowekwa kuhakikisha wananchi wanaendelea kupata huduma za kimahakama bila kukatizwa hata wakati wa mvua za El Niño.

Kwa upande wake, Jaji Mkuu George Masaju amempongeza Waziri Ulega kwa kuendelea kuaminiwa na Rais Dkt. Samia, akimhakikishia ushirikiano wa dhati kutoka muhimili huo na kubainisha kuwa ushirikiano kati ya Mahakama na Wizara ya Katiba na Sheria ni takwa la kikatiba linalolenga kuboresha utoaji wa haki.

Aidha, Jaji Masaju ameipongeza wizara hiyo kwa kuendelea kutoa huduma mbalimbali kwa wananchi, zikiwemo huduma za msaada wa kisheria na mpango maalum wa “Sema na Waziri” unaowezesha wananchi kupiga simu katika Kituo cha Huduma kwa Wateja cha Wizara na kuwasilisha malalamiko yao.

Naye Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Dkt. John Jingu amefafanua kuwa mikakati ya dharura imewekwa wazi kukabiliana na changamoto za hali ya hewa, ikiwemo matumizi ya mifumo ya kidijitali kuhakikisha haki inatolewa kwa wakati na kwa urahisi.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!