Latest Posts

TRUMP NA ZELENSKY KUKUTANA, JE, AMANI UKRAINE INAWEZEKANA?

Rais wa Marekani, Donald Trump, amesema ana “heshima kubwa” kwa Rais wa Ukraine, Volodymyr Zelensky, saa chache kabla ya mkutano wao katika Ikulu ya White House.

Mazungumzo haya yanafanyika baada ya utawala wa Trump kushangaza washirika wake wa Magharibi kwa kufanya mazungumzo ya kwanza ya ngazi ya juu na Moscow tangu Urusi ilipoivamia Ukraine zaidi ya miaka mitatu iliyopita.

Awali, Trump alionekana kumlaumu Zelensky kwa kushindwa kuanzisha mazungumzo ya amani mapema, akisema: “Umekuwa hapo kwa miaka mitatu. Ulipaswa kumaliza vita hivyo… Hukupaswa kuwa umevianzisha hata kidogo. Ungeweza kufanikisha makubaliano.”

Hata hivyo, Alhamisi hii, baada ya kukutana na Waziri Mkuu wa Uingereza, Sir Keir Starmer, Trump aliwaambia waandishi wa habari kuwa anatarajia mazungumzo mazuri na Zelensky na kwamba watafanya kazi kwa ushirikiano mzuri.

Katika mkutano huo, Zelensky anatarajia kupata dhamana ya usalama kwa Ukraine, ambayo inaweza kusaidia katika makubaliano yoyote ya amani yanayoweza kufikiwa.

Wakati wa ziara yake, Zelensky pia anatarajiwa kusaini makubaliano yatakayowapa Marekani upendeleo katika sekta ya madini ya Ukraine. Trump alipendekeza kuwa uwepo wa kampuni za madini ya Marekani nchini Ukraine utakuwa kama kinga dhidi ya mashambulizi ya baadaye kutoka kwa Urusi.

Alipoulizwa kama angeomba msamaha kwa kumwita Zelensky “dikteta” hivi karibuni, Trump alisema haamini kama alitamka maneno hayo, huku akimsifu Zelensky kama mtu “shujaa sana”.

Akihitimisha, Trump alisema anatarajia mazungumzo mazuri na kwamba juhudi za kufanikisha amani kati ya Ukraine na Urusi “zinaendelea kwa kasi kubwa”.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!