Latest Posts

VIJANA WATAKIWA KUTOIGA KILA WANACHOKIONA KWENYE MITANDAO YA KIJAMII

Vijana nchini wamendelea kusisitizwa kuepuka kuiga kila wanachokiona kwenye mitandao ya kijamii nakushauriwa kujitunza kwa kuzingatia mila na tamaduni za kitanzania zinazofaa.
Hayo yameelezwa na Naibu Katibu Mkuu  Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Wilson Mahela katika mkutano wa wadau wanaotekeleza Afua za Vijana Balehe nchini (NAIA)kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii,Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum unaofanyika kuanzia 31 Oktoba hadi 01 Novemba ,2024 Mkoani Dodoma.
Akifungua mkutano huo,  Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera ,Bunge na Uratibu  Dkt.   Jim Yonazi  ametoa rai kwa wadau wote wanaohusika na masuala ya vijana balehe kufahamu kwamba ili kuwa na Taifa imara la leo na baadae ni vema kuwekeza katika kutatua changamoto za vijana balehe leo ikiwa na maana  ya kutatua changamoto za vijana kwa ajili ya kupata taifa imara.
Mbali na hayo amesema serikali imejidhatiti kutatua changamoto zinazowakumba vijana balehe kwa kuweka mazingira salama na rafiki kwa vijana kupitia afua mbalimbali zinazowawezesha vijana kufikia malengo yao na utimilifu wao  kwa ujumla.
“Kaulimbiu  ya mkutano huu inayosema Utatuzi wa Changamoto za Vijana balehe kwa taifa imara inachechemua utekelezaji wa Ajenda  hii kwa upana wake kwa kuwa ndiyo pekee yenye uwezo wa kukabiliana na changamoto hizo za vijana kwa sasa hivyo ni matumaini yangu kuwa kupitia mkutano huu, mtapata fursa ya kujadili kwa undani kuhusu changamoto zinazohusu vijana balehe kwa kutumia uzoefu wa utekelezaji wa Ajenda hii kwa kipindi cha miaka mitatu.” Amesema Dkt. Yonazi.
“Utekelezaji wa Ajenda umejikita katika nguzo kuu 6 za ambazo ni kuzuia maambukizi ya VVU, kutokomeza mimba za utotoni, kutokomeza ukatili wa kimwili, kingono na kisaikolojia, kuboresha hali ya lishe, kuhakikisha wavulana na wasichana wanabaki shule kukamilisha mzunguko wao wa elimu, na kuwaendeleza vijana katika ujuzi na ufundi ili wapate fursa ya kujiari na kuajiriwa.” Amesema Dkt. Yonazi
Naye Naibu Katibu Mkuu wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Wakili Amon Mpanju amesema serikali inatambua  juhudi za  Mashirika ya Kimataifa na Mashirika Yasiyo ya Kiserikali yaliyoanzisha miradi mbalimbali kwa ajili ya kuhakikisha kwamba Vijana Balehe wanapata huduma rafiki za afya, elimu ya afya ya uzazi na kupata ujuzi na maarifa ya kuwafanya vijana wamudu maisha yao.
“Mafanikio haya hayajaja hivi hivi, bali ni jitihada kubwa mlizofanya ninyi Wadau wa Maendeleo kwa kushirikiana na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania aliyeunda Wizara hii ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, hivyo nachukua  fursa hii kuwapongeza kwa dhati kwa ushirikiano huo mlioonesha na kufanikisha malengo ya Ajenda hii.” amesema Wakili Mpanju

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!