Latest Posts

VIONGOZI WAHIMIZWA KUWEKA MKAZO WATU KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA

 

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu Mhe. William Lukuvi, ametoa rai kwa viongozi wa vyama vya siasa, viongozi wa dini, viongozi wa kimila na viongozi wengine kushirikiana katika kuhimiza wananchi kwenda kujiandikisha kwa sababu ni haki yao.

Wito huo umetolewa leo tarehe 11/10/2024 wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Baraza la Vyama vya Siasa uliofanyika katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma na kuhudhuriwa na viongozi wa vyama Siasa.

Ameeleza kwamba, haki ya mtu kujiandikisha inabaki pale pale awe mwanachama wa chama cha siasa au bila kuwa mwanachama wa chama cha siasa.

Waziri Lukuvi amesema, “tukijumlisha wanachama wetu wote kuna watu wanabaki ambao hawako kwenye fungu lolote  katika vyama hivi vya siasa 19, lakini bado tunao ushawishi wa kutumia sauti zetu kuhimiza  wananchi wote wenye umri wa kujiandikisha wajiandikishe  na hatimae watumie nafasi hiyo kupiga kura”

Pia Waziri Lukuvi amesema wao kama viongozi wa vyama vya siasa kwa pamoja wanao wajibu wa kuufanya uchaguzi uwe mzuri.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha (UDP) Mhe. John Cheyo amesema kuna changamoto moja ya matumizi ya muhuri wa chini ambao bado haieleweki vizuri, nadhani sisi kama wadau wa siasa tunayo nafasi kukubaliana kwa kuwa na kauli moja ya kusimamia uchaguzi kulingana na kanuni na sheria ambazo tumejiwekea.

“Tunadhamira ya kuwa na uchaguzi huru na haki kwa kila mmoja wetu na kama ilivyoelezwa na Waziri Lukuvi na hiyo ndiyo dhamira ya Mhe, Rais. Dkt. Samia Suluhu Hassani,” alisema Mhe. Cheyo

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!