Baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Tundu Lissu kujenah hoja za kwa nini hana kesi ya kujibu katika shauri la uhaini linalomkabili ambalo lipo Mahakama Kuu Masjala Ndogo Dar es Salaam upande wa Jamhuri kupitia Wakili wa Serikali Mkuu Nassoro Katuga uliieleza mahakama kwa nini wanaamini anayo kesi ya kujibu
Katuga ameeleza hayo akizingatia marejeo ya kesi mbalimbali juu ya viini vitatu katika kuthibitisha mtu ana kosa la uhaini ikiwa kiini cha kwanza cha kwamba yeye ni raia na ni mtiifu kwa Jamhuri ya Muungano ni kwamba kiini hicho amekiri kuwa yeye ni mttifu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jambo la pili ni kuhusu kutengeneza nia ya kuchochea Umma kuzuia uchaguzi wa 2025 kwa nia ya kuitisha serikali akieleza kuwa
kama maneno ya kwenye hati ya mashtaka yanahitaji utetezi akitaja maneno kama tutazuia uchaguzi tatauvuruga uchaguzi tutakinukisha haya ni maneno ambayo ukiangalia mahakama inaweza ikamwambia ajitetee nayo.
Anaeleza kuwa maneno haya ya kwenye mashtaka yamethibitishwa na mashahidi wengi wa Jamhuri na pia aliyekuwepo kwenye tukio aliyasikia na kwamba haya maneno ni ambayo yalikuwa na nia ya Kuchoche uma.
Kuwa maneno haya yanaweza yakatafsiriwa kutoka vyanzo mbalimbali kama ukisoma Oxford Dictionary na Second edition lilitafsiriwa neno kutishia ni kumfanya mtu awe na woga kumlazimisha mtu au kufanya mtu afanye kitu fulani kwa uwoga na kwa mujibu wa hati ya Mashtaka na Kwa mujibu wa Kifungu cha 39 cha Kanuni ya Adhabu ni kwamba mtu yeyote atakayetengeneza nia ya kufanya jambo fulani kwa ni ya kuitishia serikali aidha serikali imetishika au haijatishika basi utakuwa umetenda kosa chini ya kifungu hicho cha 39(2)(d).
Kuhusu nia ya kuitisha serikali Katuga amesema hayo yameelezawa na shahidi PW1,PW3 na PW 16 ambapo PW3 na PW16 wanasema maneno ya Lissu tutazuia uchaguzi yanaelenga kuitisha serikali kwa maana kwamba serikali ya Jamhuri ni mlinzi wa sheria na wakasema na kutishia kuvuruga sheria ni kutishia serikali yenye majukumu ya kuilinda sheria wakieleza kuwa Uchaguzi Mkuu wa 2025 ulikuwa kwa mujibu wa katiba na kuutishia kuvuruga ni kuvunja katiba na sheria na wakaeleza kuwa serikali ni mlinzi wa amani katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kitendo cha Lissu kutoa matamshi yake na kuchapisha kwa umma ni kutishia kuanzisha vurugu kuzuiwa wataakaoenda kupiga kura na kuwapiga mawe watakaoenda kupiga kura manejo ambayo yamsemwa na PW3.
Shahidi huyo alisema kuwa wanaenda kupiga watu mawe na kuwa kutishia kuvuruga amani ni kutisha serikali akieleza kuwa haijatishwa Mahakama wala Bunge bali ni serikali na kwa tafsiri hiyo hoja hiyo inamtaka Lissu alete utetezi.
Kuhusu hoja ya kuchapisha Katuga alieleza Mahakama kuwa kwa mujibu wa hati ya mashtaka mshtakiwa alithibitisha nia kwa kutoa maneno hayo mtandaoni na jamhuri imeleta mashahidi wa kutosha kuwa alichapisha mtandaoni na kuwa kitendo cha kutoa maneno yale ni kitendo ambacho kinaonyesha hakipiganiwi mahakamani kwamba nimetoa au sijatoa maneno hayo labda kuwa maneno hayo ni uhaini.
Kitendo cha kutoa maneno hayo kimethibitishwacna mashahdii wa jamhuri kuanzia PW1,PW2 na mashahdii wengi mpaka PW16 suala linabaki kuwa kama alichapisha na maneno hayo yamethibitishwa na shahidi PW17 ambaye alikuwa eneo lile.
Katuga anaeleza suala la kuchapisha limezungumzwa na mashahidi wa Jamhuri kuanzia shahidi wa kwanza mpaka wa 17 wote kwa kiwango kikubwa wakisema waliona maneno hayo katika mtandao wa Youtube akaunti ya Jambo TV.
Jamhuri imesema wanafahamu walijaribu kuleta video lakini Mahakama iliamua kwa haki kuikataa video hiyo akieleza kuwa video hiyo ni ushahidi wa kielektroniki huku akiendelea kuieleza Mahakama kwua kutokuwepo kwa ushahidi wa kimaandishi/nyaraka hakumaanishi ushahidi wa maneno hauna nguvu, kuwa kisheria ushahidi wa kinyaraka na ushahidi wa maneno wote uko sawa.
“Haitakua sawa kisheria kusema ili ushahidi wa mdomo ukubaliwe pawepo ushahidi wa nyaraka” alisema Katuga
“Mashahidi wanasema kwa kitendo chako cha kuongea kwenye vyombo vya habari ulikusudia maneno yako ya kuitisha serikali ya kuchochea yaufikie umma.”
Baada ya hoja za pande zote mbili Jaji Dunstan Ndunguru ambaye ni kiongozi wa jopo la Majaji watatu wanaosikiliza kesi alisema jopo hilo litapitia hoja zote pamoja na ushahidi na ijumaa Agosti 21, 2026 uamuzi wa kama Lissu ana kesi au lah utatoka.