Latest Posts

WABUNGE KENYA WAANZA MCHAKATO WA KUMUONDOA NAIBU RAIS GACHAGUA

Wabunge nchini Kenya wanatazamiwa kuwasilisha hoja ya kumg’oa madarakani Naibu Rais Rigathi Gachagua katika bunge la taifa baadaye leo.

Kiongozi wa Wengi na Mbunge wa Kikuyu Kimani Ichung’wah alithibitisha kuwa hoja dhidi ya Gachagua itawasilishwa mbele ya Bunge saa nane unusu leo kwa saa za Afrika mashariki.

Uwasilishaji wa hoja hiyo utahitaji kuungwa mkono na wabunge 233 na kuna taarifa zinazodai kuwa wajumbe 302 tayari wametia saini.

Wanaomshitaki Gachagua wanadai kuwa amekiuka Kifungu cha 10 cha katiba, wakisema matamshi yake hadharani yamekuwa ya uchochezi na yanaweza kuibua chuki za kikabila.

Pia anatuhumiwa kukiuka vifungu vya 147, 148,174,186 na 189 vinavyozungumzia mwenendo na wajibu wake kama msaidizi mkuu wa Rais.

Pia atajitetea dhidi ya madai ya kujipatia mali kwa ufisadi na kutumia pesa za walipa kodi kwa njia isiyo halali. Mali hiyo inasemekana kusambazwa katika kaunti za Nyeri, Nairobi na Kilifi.

Ikiwa hoja hiyo itakamilika, spika wa bunge la taifa Moses Wetangula atawasilisha azimio hilo kwa spika wa bunge la seneti Amason Kingi ndani ya siku mbili ili achukuliwe hatua.

Hoja ya kumuondoa madarakani Gachagua inakuja huku kukiwa na uhusiano mvutano baina yake Rais William Ruto. Viongozi hao wawili wamekuwa wakitupiana lawama kila mmoja akidai mwenzake anakwamisha utendaji wa mwenzake.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!