Wakala wa Vipimo (WMA) umewataka wafanyabiashara wanaotumia mizani kuacha dhuluma na kupunja kwani hata vitabu vya dini vinazungumzia haki kwenye vipimo.
Agizo hilo limetolewa leo Jumanne Machi 25, 2025 na Afisa Mtendaji Mkuu wa wakala wa vipimo(WMA) Alban Kihulla wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafanikio na mwelekeo wa Wakala hip katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita katika Ofisi za Idara ya Habari – MAELEZO, Jijini Dodoma.
Kihulla amesema Kuna baadhi ya wafanyabiashara wamekuwa wakitumia mizani isiyo sahihi wengine wakipunguza mawe ya mizani ili kupata faida na kuwapunja wateja.
Aidha, Afisa huyo amesema ili kutimiza azima ya kumlinda mlaji Wakala imepewa dhamana ya kusimamia Kisheria matumizi sahihi ya vipimo Kwa kutekeleza majukumu ya kuhakiki vipimo vyote vinavyotumika kwenye sekta mbalimbali.
Hata hivyo , amebainisha kuwa katika kipindi Cha miaka minne ya Serikali ya awamu ya sita Wakala ilipanga kuhakiki vipimo Milioni 3,923,652 vitumikavyo katika sekta mbalimbali nchini imefanikiwa kuhakiki vipimo 3,668,149 sawa na Asalimia 94 ya Malengo.