Latest Posts

LISSU: KINGAI AMEKATAA KUNITETEA, AMESEMA ATASHANGILIA NIKIKUTWA NA HATIA

Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Ramadhani Kingai, aliyetarajiwa kufika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, leo Septemba 18, 2026, kutoa ushahidi kama shahidi wa sita wa upande wa utetezi katika kesi ya uhaini namba 19605/2025 inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, amekataa kuwa tayari kutoa ushahidi huo.

Akizungumza mbele ya jopo la majaji watatu wakiongozwa na Jaji Dunstan Ndunguru, Tundu Lissu ameeleza kuwa alikutana na DCI Kingai na kuzungumza naye kuhusu maeneo aliyotakiwa kuyatolea ushahidi, lakini afisa huyo alimueleza wazi kuwa hayuko tayari kutoa ushahidi kwa upande wa utetezi.

Lissu, ameongeza kuwa Kingai amedai kuwa hata mashahidi wengine wawili waliotakiwa kupewa wito wa mahakama Jenerali Jacob Mkunda na Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP) Camilius Wambura watakuwa na msimamo huo huo wakirejea nchini.

Kutokana na mazingira hayo, Lissu ameiomba mahakama kumruhusu kufunga ushahidi wa upande wa utetezi, kwani hawezi kuwalazimisha mashahidi hao, huku akiomba ipangwe tarehe maalum kwa ajili ya kusikiliza hoja za mwisho (Final Submissions) za pande zote mbili.

Kwa upande wake, upande wa mashtaka uliungana na ombi hilo huku ukihoji kama uwasilishaji wa hoja hizo utafanyika kwa njia ya mdomo au maandishi, ambapo Lissu alifafanua kuwa utakuwa wa mdomo kutokana na yeye kuwa gerezani na kukosa zana ambazo upande wa Jamhuri wanazo.

Mahakama imeahirisha shauri hilo na kupanga kusikiliza hoja za mwisho kwa njia ya mdomo siku ya Jumatano, Septemba 23, 2026.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!