Latest Posts

WAHITIMU NDC KUKABILIANA NA CHANGAMOTO ZA KIUSALAMA

Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Balozi Meja Jenerali Wilbert Ibuge amewahakikishia Watanzania kuwa mafunzo yanayotolewa na chuo hicho kwa washiriki kutoka ndani na nje ya nchi yamewawezesha wahitimu kuwa na uwezo wa kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazoweza kujitokeza katika maeneo yao.

Balozi Meja Jenerali Ibuge ameyasema hayo Jumatatu Machi 10, 2025 Jijini Dodoma alipoongoza ujumbe wa kozi ndefu ya NDC kundi la 13 la mwaka 2024/2025 katika ziara ya mafunzo kwa vitendo ya kutembelea vyombo vya ulinzi na usalama ambapo amesema washiriki hao wanaandaliwa ili kukabiliana na matishio ya kiusalama katika nyanja mbalimbali

Amesema mbali na kuwaandaa wataalam kwa ngazi za kiusalama pia wana jukumu nyeti la majukumu ya usalama wa nchi.

“Chuo chetu ni changazi ya kimakakati na tunachokizungumzia ni usalama kwa ngazi ya kimkakati lengo siyo ule usalama ambao mtu ukisema unajua ni Jeshi, Polisi, TSS ndiyo hiyo ni sehemu yake lakini ni zaidi ya hapo kila kitu kinahusu usalama,” ameeleza na kuongeza,

 

“Mabadiliko ya tabia ya nchi, magonjwa yakuambukiza lakini pia Mhe Rais anazungumzia sana Suala la nishati safi, suala la uhimilivu wetu kwenye tabia ya nchi ili tuweze kuhakikisha tunapunguza madhara ya tabia ya nchi hiyo yote ni sehemu ya usalama wa taifa,”

Aidha ameongeza kuwa “kuna kozi fupi ambayo tumeipanga   awamu wakiwemo taasisi binafsi na tunalenga viongozi na watoa maamuzi ili Muunganiko wa sera za serikali napia yanayofanyika kwenye sekta binafsi yawe na muunganiko ule wa usalama wa Taifa kwa sababu usalama wa taifa siyo serikali peke yake mpaka sekta binafsi,”

Kwa upande wake Katibu Mkuu Balozi Dr. Samwel Shelukindo amesema kwa matokeo ya diplomasia bora chuo hicho kinaendelea kuwa cha kimataifa.

Naye Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Rajabu Mabele, amesema ugeni huu una maana kubwa kwao ikiwemo kuwafunza mbinu za kisasa za ulinzi.

Ziara hiyo ya mafunzo kwa vitendo ya kutembelea vyombo vya ulinzi na usalama ina washiriki 61, na itakuwa ya siku tano katika mkoa wa Dodoma, ikianzia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ambapo washiriki wamepatiwa wasilisho kuhusu Sera ya Mambo ya Nje.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!