Latest Posts

WANANCHI WAHIMIZWA KUTHAMINI JITIHADA ZINAZOFANYWA NA SERIKALI

Wananchi wametakiwa kuunga mkono, kuthamini jitihada na mchango wa serikali katika kuwaletea maendeleo wananchi wake kwenye sekta mbalimbali.

Akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani mkoani Mtwara Shadida Ndile amesema tangu kupata uhuru taifa limepiga hatua kubwa katika sekta mbalimbali kama vile sekta ya elimu, kilimo, barabara, afya na utoaji wa mikopo kupitia asilimia 10 za mapato ya ndani ya halmashauri.

“Kama manispaa ya Mtwara Mikindani jitihada za Serikali na chama cha mapinduzi ccm katika maeendeleo zinaonekana waziwazi, kwani sekta ya usafirishaji, kilimo, Elimu na afya hivi sasa zimeboreshwa ukilinganisha na hapo nyuma kabla ya uhuru, hali ambayo tunapaswa kujivunia na kuunga mkono serikali ya Dkt Samia Suluhu Hassan.”Amesema Ndile

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi CCM wilaya ya Mtwara Mjini, Fadhili Mrami amesema mchango wa chama hicho katika kuleta mageuzi kwenye sekta mbalimbali nchini ni mkubwa ikiwemo sekta ya afya ambapo kwa sasa matibabu ya maradhi makubwa kama ugonjwa wa figo yanapatikana kwenye kila halmashauri vilevile mtwara kuna Hospitali ya Kanda ambayo ni tunu na neema kwa kila mkazi wa mtwara ukilinganisha na hali kabla ya uhuru.

Naye Emiliana Renatus Waziri wa serikali ya Wanafunzi Chuo cha Utumishi Wa Umma kilichopo kwenye manispaa hiyo amekiri uwepo wa neema na mchango wa serikali kwenye sekta mbalimbali, kama vile sekta ya elimu na kilimo huku akifurahishwa na hatua iliyopigwa kama taifa kwani hivi sasa Tanzania inaadhimisha miaka 63 ya uhuru ikiwa imepiga hatua mbele kwenye sekta mbalimbali za maeendeleo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!