Latest Posts

WASAMBAZAJI WA GESI YA KUPIKIA WAOMBWA KUFUATA MASHARTI YA LESENI ZAO

Wasambazaji na wafanyabiashara wa gesi ya kupikia majumbani (LPG) mkoani Mtwara wametakiwa kuwa na leseni na kufanya biashara hiyo kwa kufuata masharti ya leseni zao.

Akizungumza Mei 8, 2025, Meneja wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji Nchini (EWURA) Kanda ya Mashariki Mhandisi Nyirabu Musira kwenye mafunzo ya siku moja yaliyowakutanisha wasambazaji na wafanyabiashara wa gesi ya kupikia majumbani mkoani humo.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Manispaa ya Mtwara Mikindani yeye lengo la kukumbushana mambo muhimu ya kuzingatia wakati wa usambaji wa gesi hiyo.

Amesema EWURA ina wajibu wa kuhakikisha kuwa usambajazi wa gesi ya kupikia majumbani unafanyika kwa njia ambazo ni salama na kufuata taratibu ambazo EWURA inaziweka kwenye leseni ambazo wanazitoa kwa wazambazaji.

“Kwa siku za hivi karibuni tumeshuhudia matukio ya ujazaji haramu wa mitungi ya gesi ya kupikia majumbani.”Amesema Musira

Amepongeza kuwa “unakuta mfanyabiashara wa mtungi mkubwa wa gesi anajaza kwenye mtungi mdogo pasipo kutumia njia sahihi na hii ni changamoto kwasababu wanapofanya hivi wanaweza kusababisha moto kutokea na unaweza kuunguza miundombinu na kuhatarisha maisha ya watu”

 

Hata hivyo amewasihi watumiaji wa gesi hiyo kuhakikisha wananunua gesi kwa wakala mwenye leseni ya EWURA na wanapaswa kuhakikisha muuzaji anakuwa na mzani kwa ajili ya kupimia mtungi na kujiridhisha namba iliyoandikwa kwenye mtungi na inayosoma kwenye mzani ni sawa.

Kwa upande wao baadhi ya wasambazaji wa biashara hiyo aikiwemo Laurent Said wameipongeza EWURA kwa kuwapa elimu hiyo na kuahidi kwenda kuitekeleza ipasavyo.

Latest Posts

Don't Miss

Stay in touch

To be updated with all the latest news, offers and special announcements.

error: Content is protected !!