Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Wanawake Duniani, wasichana wanaosoma katika vyuo mbalimbali hapa nchini wamemwomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassani kuanzisha taasisi ya kutoa elimu ya afya ya uzazi ili kukabiliana na tatizo la maambukizi ya UKIMWI, mimba zisizotarajiwa na magonjwa ya zinaa kwani kukosekana kwa elimu hiyo kunasababisha wasichana wengi washindwe kutimiza ndoto zao wanapokua vyuoni.
Akizungumza jijini Mwanza Makamu Mwenyekiti wa kampeni ya Mama Asemewe Taifa, Verynancy Mrema amesema jina la Binti wa Leo Samia wa Kesho Foundation ndilo lililopendekezwa kuwakilisha taasisi hiyo.
Kwa upande wake Katibu wa Idara ya Mabinti na Uwezeshaji wa Kampeni ya Mama Asemewe taifa, Benedicta Mseko amesema kutokana na kuwepo changamoto hiyo, kampeni hiyo imeandaa kongamano la Binti wa Leo Samia wa Kesho ili kuwafungua fikra watoto wa kike na kuwajengea uwezo wasichana ili wafikie ndoto zao.